MKUU WA WILAYA YA GAIRO APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI HOLELA WA MADINI YA RUBY

Madini ya vito aina ya Ruby ni kati ya madini yanayopatikana Wilaya ya Gairo.

Image result for ruby

Madini hayo yameanza kuchimbwa na mzungu (jina linahifadhiwa) tangu mwaka 2010 katika kijiji cha Chogoali, Kata ya Iyogwe Wilayani Gairo.

Ad

Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi na wazee maarufu madini hayo yalichimbwa kuanzia mwaka 2010 na baadae mwaka 2015 yalisitishwa. Katika kipindi cha uchimbaji walipakia zaidi ya viroba 20.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama (W), wataalamu kutoka Ofisi ya Afisa Madini Kanda, wataalamu wa mazingira Halmashauri ya #Gairo, Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji Kata na Kijiji walifanikiwa kufika eneo la tukio mara baada ya kufanya mkutano ambapo elimu kuhusu rasilimali ya madini ilitolewa kwa wananchi.

Mhe. Mchembe na wataalamu walifika eneo la machimbo ambapo waliokota udongo wenye makinikia ya madini ya ruby katika punje ndogo ndogo.

Wazee hao ambao wanataka kuuendesha mgodi huo kwa kufuata taratibu walieleza jinsi ambavyo maji yalianza kutoka kwa wingi kwenye mwamba na ndio uliwazuia kuchukua madini hayo. Mpaka sasa wamechimba mita 30.

Wazee hao waliomba ufadhili wa mitambo na teknolojia waweze kuchukua madini hayo kwenye mashimo mawili ambayo yana mkondo wa madini ya ruby kama ambavyo wataalamu wa madini walibainisha. Pia mashimo hayo yamezungukwa na nyuki ingawa hawaumi.

Mhe. Mchembe aliwaagiza wazee hao waende Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro wakafuate taratibu zote za kisheria waweze kumiliki mgodi huo ambao ulionesha kuwa hauna mtu.

Mhe. Mchembe na wajumbe wa KUU (W) wanaendelea na ziara ya kubainisha maeneo ya uchimbaji haramu sambamba na utoaji wa elimu hasa katika Sheria zote za Madini.

Lengo kuu ni ili Watanzania wafaidike na rasilimali hii kama Rais wa JMT Mhe. Dr. John Pombe Magufuli anavyosisitiza kila wakati.

Mwisho Mhe. Mchembe aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaompa katika kutoa taarifa za uchimbaji haramu kona zote za Gairo.

#Gairo Maendeleo Fasta kwa Mwendo Mdundo

Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI MKOANI SHINYANGA YAKUSANYA  BILIOINI 1.5 KAMA KODI YA MRABAHA NA ADA YA UKAGUZI KUTOKA KWA WACHIMBAJI

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph kumburu amesema kuwa utaratibu mzuri uliowekwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *