DSM: “Watu 11,669 wamekamatwa kwenye kampeni ya usafi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam” Paul Makonda

Watu 11,669 wamekamatwa kwenye kampeni ya usafi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kati yao, watu 6,667 walipigwa faini na kuwezesha kupatikana kwa fedha kiasi cha Sh346 milioni, ambacho nusu yake imetumika kuwalipa mgambo ambao wanatekeleza kampeni hiyo.

Ad

Akizungumza kwenye mkutano na wadau wa usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam, Makonda alisema lengo la kampeni hiyo siyo kujipatia fedha bali kuhakikisha jiji linakuwa safi.

“Nina imani hawa mgambo watafurahi watu waendelee kuwa wachafu kwa sababu wanajipatia ajira. Lakini sisi kama Serikali, lengo siyo kujipatia kipato, lengo siyo kumshitaki mtu, lengo ni kuwataka watu wawe wasafi,” alisema Makonda.

Mkuu huyo wa mkoa alisema watu 4,043 waliachiwa huru, watu 376 walidhaminiwa, watu sita walifikishwa mahakamani na wengine 2,213 walipewa adhabu ya kufanya usafi.

Kuhusu mgambo wanaopiga wananchi, Makonda alisema analaani vitendo hivyo kwani siyo lengo la kampeni hiyo kukomoa watu bali kusimamia usafi katika mkoa wake.

Alisema mgambo hawana mamlaka yoyote ya kumpiga raia, badala yake wanatakiwa kumfikisha mwananchi anayewapinga kwenye ofisi za serikali ya mtaa au kata.

Alisema watendaji wa mtaa na kata wana wajibu wa kumchukulia hatua za kisheria mgambo anayekiuka taratibu za kazi yake.

“Tulipopata taarifa kule Bunju mgambo wamewapiga wananchi, polisi waliwachukua wahusika, wakawafikisha Mahakamani, hawakuwa na dhamana, sasa wako Segerea,” alisema.

Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: HALFA YA KUWAPONGEZA ASKARI WA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DSM 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *