MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI SARAH COOKE

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.

Pamoja na mambo mengine Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alimpa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza, atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu yenye lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia unaohusu masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori utakaofanyika London, Uingereza mwezi Oktoba.

Ad

Aidha Balozi Cooke alimjulisha Mhe. Makamu wa Rais utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Aprili 2018, jijini London, Uingereza.

Ad

Unaweza kuangalia pia

NINAWASIHI MUWE NA SUBIRA WAKATI SERIKALI IKIIMARISHA MIFUMO YAKE YA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *