UZINDUZI WA KIKOSI KAZI KITAKACHOTAFITI, KUSHUGHULIKIA NA KUTATUA TATIZO LA VIUMBE WAGENI/VAMIZI KATIKA MAZINGIRA, AFYA NA USTAWI WA JAMII YA TANZANIA.

MAKAMU WA RAIS;Elimu inahitajika kuzuia viumbe wageni/vamizi

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni vema kama nchi kujipanga mapema kuhakikisha kwamba viumbe vamizi hawaendelei kushamiri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye gharama kubwa za kukabiliana na janga hilo hapo baadaye.

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Kikosi Kazi cha Kutatua Changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na kwamba viumbe hawa ni janga la kiuchumi, kimazingira na kiafya lakini bado halijashughulikiwa kikamilifu hususani katika elimu ya kuzuia viumbe hawa na kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana nalo” alisema Makamu wa Rais.

Ad
MHE. JANUARY YUSUF MAKAMBA, NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA.
Akihutubia katika uzinduzi wa kikosi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/vamizi ambapo amesema aligua tatizo la viumbe vamizi kushamiri nchini baada ya kufanya ziara na kukuta athari za mimea na viumbe vamizi zimekuwa kubwa na tishio kwa wananchi.

Amesisitiza kuwa Janga hili si la sekta moja na linapaswa kufanywa na sekta zote nchini ili kukabiliana nalo kikamilifu. 

Amezitaka Sekta zote na Taasisi zifanye kazi kwa pamoja kwa kupeana taarifa na mikakati ya kukabiliana na changamoto hii,na kutaka ushirikishwaji wa wadau wote wakiwemo, Halmashauri za wilaya ,Wizara za kisekta, Serikali za Mitaa, Asasi za Serikali na zisizo za Serikali, Sekta binafsi pamoja na wananchi pamoja na vyombo vya habari.

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kikosi Kazi cha Kutatua Changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini mara baada ya uzinduzi wa Kikosi kazi hicho uliofanyika kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega

Akitoa rai kwa waliochaguliwa kuunda Kikosi Kazi cha Kitaifa, Makamu wa Rais alisema “Tambueni kuwa mmepewa jukumu kubwa la kulisimamia suala hili kikamilifu,kafanyeni kazi kulingana na Hadidu za Rejea tutakazo wakabidhi ili mwisho wa yote kuwe na matokeo chanya ya kazi mliyopewa na Taifa”.

 

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa aligundua tatizo hili mara baada ya kufanya ziara yake ambapo amekuta athari za mimea na viumbe vamizi zimekuwa kubwa na tishio kwa wananchi hivyo kuona kuna kila sababu ya kuanza kulishughulikia.

Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 18 kilichozinduliwa kitaongozwa chini ya Mwenyekiti Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *