WAZIRI MKUU – BENKI KUU SASA ITADHAMINI MIKOPO YA MTAJI YA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO KATIKA MABENKI!

WAZIRI MKUU MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA
Waziri Mkuu akimsikiliza mtaalamu wa BoT akielezea namna ilivyojipanga kudhamini machimbaji wadogo wadogo. Katikati yao ni Waziri wa Madini Mhe. Anjela Kairuki

“Leo nimepita eneo nimekuta Bank Kuu.. na wenyewe Benk ya Biashara NBC.. wananiambia, sisi tuko tayari kutoa mikopo kwa wajasiliamali (wa Madini); ili wanunue mitambo, wanunue vifaa vingine vya kusaidia kuchimba.. lakini pia na kuboresha.” – Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

30/09/2018, Geita

MHE. KASSIM MAJALIWA, WAZIRI MKUU WA TANZANIA

“Benki Kuu wanasema, ni nyie tu (wachimbaji wa madini) mnachelewa kwenda kuomba mikopo.” Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

30/09/2018, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Tanzania.
Waziri Mkuu akihutubia wachimbaji wadogo wadogo, viongozi wa Wizara ya Madini pamoja na wadau wa sekta ya madini nchini katika hitimisho la maadhimisho ya Maonesho ya Madini yaliyofanyika Geita tarehe 30/09/2018.

“Na sio lazima uende Benk Kuu.. nilimuuliza swali, we benki Kuu uko Mwanza; Huyu mchimbaji mdogo yuko yuko Nyarugusu anakupataje? Wakaniambia, sio lazima aje Benki Kuu. Kila benki NMB, CRDB, NBC na benki nyingine yoyote ukienda..ukienda mikopo kwa ajili ya madini.. Benk Kuu itakudhamini..” – Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

30/09/2018, Geita.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
Mhe. Waziri Mkuu alipokuwa akihutubia wadau wa sekta ya madini katika hitimisho la maonesho ya madini mkoani Geita

“Fomu utakayopewa kujaza (kuombea mkopo katika benki husika) itakuonyesha kipengele cha kwenda Benki Kuu kwenda kukudhamini; Kwahiyo mnakopesheka! Tunachozungumza ni cha uhakika.. tumezungumza na mabenki sasa yajiimarishe kukopesha wajasiliamali wadogo wadogo, wachimbaji wadogo wadogo kwenye sekta ya Madini na wafanyabiashara wengine. Msihofu; Nenda mkakope.. ndio njia pekee ya kupata mtaji wa Uhakika.” – Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa

30/09/2018, Geita.

 

Unaweza kuangalia pia

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUKUA NA KUIMARIKA

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.