WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA

 • Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka watumishi walio kwenye Wizara yake hiyo kupitia mafunzo ya Jeshi Usu ili kujiimalisha zaidi katika kutokomeza vitendo vya ujangili wa Maliasili zilizopo sehemu mbalimbali hapa nchini.
 • Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo Novemba 24, 2018 wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu 289 katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii kwenye Mahafali ya 54 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori- Mweka, Wilayani Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

WAZIRI MALIASILI NA UTALII

 • Akielezea suala la kupata mafunzo kwa watumishi hao, amesema suala hilo la uhifadhi ni la kudumu hivyo ni vyema watumishi hao kujiandaa katika ulinzi wa Maliasili za Taifa.
 • Dkt Kigwangalla amesema mifumo wanayotengeneza ikiwemo Jeshi Usu lazima ifanye kazi imara na iwe madhubuti ili kusaidia kulinda Malisili zilizopo kwani hali ya uvamizi wa wananchi na waalifu wa Maliasili za taifa ni kubwa.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---267

 • “Kama Serikali tuna nia na dhamira ya dhati ya kulinda na uhifadhi Maliasili tulizonazo ambazo ni urithi sio tu kwa watoto wetu hapa Tanzania, lakini ni urithi wa vizazi na vizazi vya Dunia yote” amesema Dkt. Kigwangalla.
 • Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa wiki mbili kuanzia Novemba 24, kwa taasisi nne zilizo chini ya Wizara hiyo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kila kutoa Shilingi Milioni 100 ilikuchangia ujenzi wa jengo la Utawala na mafunzo chuoni hapo ili kuanza mara moja ujenzi wa jengo hilo jipya.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---266

 • “Kwa mamlaka niliyonayo, Nawaagiza taasisi za TFS, NCAA, TANAPA na TAWA kwa kuanzia, ndani ya wiki mbili zinazofuata kabla hatujaenda likizo ya sikukuu za Christmass, Wawe wameleta shilingi milioni 100, kila taasisi hapa Mweka. Ambapo kwa taasisi hizo nne nilizozitaja tutakuwa tumefikisha shilingi milioni 400” amesema Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo ya kuchangia Chuo hicho ambacho kimetoa viongozi na watendaji wakuu wengi wa Serikali wakiwemo wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii.
 • Aidha, Dkt. Kigwangalla ametoa wito kwa wahitimu baada ya dakika chache za kufurahia kutunukiwa cheti, waanze mawazo ya kujiajiri na kuwaajili wengine kwa kutumia elimu waliyopata chuoni hapo na kuachana na dhana ya kutembea na bahasha za kaki kutafuta kazi.
 • “Chuo hiki kikongwe. Kina sifa ya kipekee hivyo fikiria zaidi kwenda kujiajiri na pia ukawaajiri wengine baadala ya kwenda kuzunguka kwenye maofisi na bahasha za kaki.. unakuta mtu anazunguka kila ofisi hata ambayo haijatangaza nafasi za kazi. Nendeni mkajiajiri wenyewe kwa elimu mulioipata hapa” amesema Dkt. Kigwangalla.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---265

 • Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) amesema kamati yake imepokea changamoto ya miundombinu ya chuo hicho na watakaa kuona namna ya kupitisha bajeti ya chuo hicho.
 • Nape ameongeza kuwa, kwa taasisi zote za Umma na binafsi zinazojihusisha na Utalii waanze kuchukua watumishi kutoka Chuoni hapo ilikupata watumishi wazuri na utasaidia kupata bora wa shughuli za Utalii na uhifadhi.
 • Naye Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho amesema Chuo hicho kina ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati sasa wa taasisi binafsi na za Kiserikali kuendelea kutoa ajira kwa vijana wanaopikwa Chuoni hapo.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---270

 • Mahafali hayo ya 54 yalihudhuriwa pia na Balozi wa Nigeria nchini, Balozi Sahabi Dada, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho, na wengine wengi.
 • Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilianzishwa mwaka 1963 baada ya azimio la Arusha mwaka 1961 ambalo lilitaka uwepo wa watu waliopewa mafunzo kwa ajili ya kulinda na kusimamia urithi wa rasilimali za Afrika.
 • Chuo hicho ambacho huendesha mafunzo yake kwa vitendo kwa zaidi ya asilimia 60 kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 25 mwaka 1963/1964 hadi zaidi ya wanafunzi 550 mwaka 2016/2017 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na Cameroon.
 • Aidha, katika kipindi cha miaka 54 iliyopita chuo hicho kimeweza kufundisha zaidi ya mameneja wa wanyamapori 8,000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani.
 • Chuo hicho pia kimepewa tuzo na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama Kituo cha Ubora wa Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori (Centre of Excellence).
Ad

Unaweza kuangalia pia

ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi …

Oni moja

 1. Hongera mweheshimiwa kwa kazi nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *