MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI KONGAMANO KUHUSU TATIZO LA DAWA ZA KULEVYA KWA WASANII.

  • Limeandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya.
  • Limehudhuriwa wa wasanii wa fani mbalimbali.

fuatilia kongamano hili kwa kubofya link hii..

 

 

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wa meza kuu na wasanii kusimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop Tanzania Golden Jacob Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo kabla ya kuanza kuhutubia Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 

JN-4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kwa umakini Sanaa ya maigizo iliyokuwa ikionyeshwa na wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliokuwa wakionyesha madhara ya dawa ya kulevya wakati wa Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 .Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati akiingia katika Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI YA CANADA YATOA FEDHA ZA KITANZANIA BILIONI 90 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA VYUO VYA UALIMU NCHINI

Kiasi cha fedha za kitanzania bilioni 90 zimetolewa na Serikali ya Canada kupitia mradi wa  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *