Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara.

SERIKALI INASOGEZA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI – MAKAMU WA RAIS

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
SAMI-4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.
  • Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.
  • Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
  • “Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara.
  • Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.
  • Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.
MAKAMU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara.
  • Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *