• Anaitwa Flora Kihombo binti mwenye umri wa miaka 10 anayeendelea na elimu ya msingi (Darasa la Sita)

•• Ni mtoto wa nne kuzaliwa katika familia duni yenye watoto 7 ambapo kutokana na ugumu wa maisha, wazazi wake iliwalazimu muwandikisha kwenye kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu mwaka 2015 ili apate fursa ya kutimiza ndoto zake za kuwa muingizaji bora na daktari bingwa wa macho.
••• Asimulia hali halisi ya nyumbani kwao ambapo hula mlo mmoja pekee(ugali na mboga za majani) katika kipindi chote cha ukuaji wake
•••• Atokwa na machozi baada ya kuulizwa swali kuhusu nyumba ya familia yao. Asema ilibomoka kwa mvua kali mwaka jana 2018 na toka wakati huo mpaka sasa familia imejihifadhi kanisani.
••••• Asema fedha alizozipata baada ya kutwaa Tuzo ya Muingizaji Bora wa Kike – SZIFF 2019, atazitumia kujenga nyumba ya kuishi familia yake sambamba na kununua mahitaji ya nyumbani kama chakula na nguo kwaajili ya baba na mama yake.
•••••• Inafaa kutafakari na kujifunza; Sisi si wastahili zaidi ya wengine
maana #SisiNiTanzaniaMpyA+
Fuatilia mahojiano mafupi yaliyofanywa mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji tuzo hizo usiku wa kuamikia Februari 23, 2019.