Muonekano wa ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katikati ya Hospitali ya Aga Khan mpaka Coco Beach.
Daraja hilo litajengwa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu, likiwa na urefu wa Kilomita 6.23 huku Kilomita 1.4 zikipita juu ya Bahari.
Daraja litalopambwa na nguzo za zege mithili ya viganja vya mikono ya binadamu litaunganisha barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach katika makutano ya barabara za Kenyatta na Toure ambapo mradi unatekelezwa kwa Sh.Bil 556.1 huku serikali ya Tanzania ikitoa Bil.49.457.
Muonekano wa ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katikati ya Hospitali ya Aga Khan mpaka Coco Beach.Muonekano wa ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katikati ya Hospitali ya Aga Khan mpaka Coco Beach.