RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASIFU MAONESHO YA 43 YA SABASABA JIJINI DAR

JK

  • Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.
JK
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa ziara yake aliyoifanya  Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  • Akizungumza  Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.
JK
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara yake aliyoifanya  Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  • Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.
JK
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Maafisa wa Idara ya Sera na Machapisho wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa ziara aliyoifanya  Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MAELEZO)
  • “Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.
  • Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *