- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahamasisha Watanzania kutembelea Wiki ya Maonesho ya Biashara ya nchi za SADC yanayoendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijjini Dar es Salaama ili kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa.
- Amesema ni fursa kubwa kwa Watanzania kuona bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yao lakini pia wakaona bidhaa zinazozalishwa na nchi nyingine ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Bara la Afrika.
- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Agosti 6,2019 baada ya kutembelea mabanda yaliyopo kwenye maonesho hayo ya SADC ambapo amefafanua kuwa ameona bidhaa za aina mbalimbali ambazo zinazozalishwa nchini zikiwa kwenye kiwango cha ubora wa hali ya juu na hivyo ameshauri Watanzania kujitokeza kwa wingi.
- “Maonesho haya ni bure,nitoe rai kwa Watanzania wafike waone namna ambavyo bidhaa za hali ya juu ambazo zimetengenezwa na Watanzania.Pia wakifika wataona bidhaa zinazozalishwa na nchi nyingine.Ni fursa kubwa kwetu Tanzania kutumia nafasi hii kutangaza biadhaa zetu za ndani,”amesema Waziri Mkuu.
- Amesema pia katika maonesho hayo kuna bidhaa mbalimbali zitokanazo na nafaka huku akutumia nafasi hiyo kueleza bidhaa hizo mbali ya kuwa kwenye maonesho watapata fursa ya kuuza bidhaa zao mwishoni mwa maonesho hayo
- Amesema ni wakati mzuri wa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuhamasisha wawekezaji wa nje kuja kuwekeza nchini Tanzania kwani mazingira ni mzuri,huku akitoa rai kwa vyombo vya habari nchini kuendelea kuitangaza nchi yetu.
- Wakati huo huo Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania kuwakarimu wageni wote ambao wamefika kwenye mikutano ya SADC na kwamba wageni wengi wameshafika na wengi e wanaendelea kuwasili.
- Pia amezungumzia umuhimu wa kutangaza vivutio vya utalii wa nchi yetu ambavyo ni vingi na ni wakati muafaka kuhakikisha utalii wetu unaendelea kuzungumzwa na kuwahamasisha wageni kwenda kutembelea ma kuona maeneo ya utalii wetu.
- Amesema nchini Tanzania kuna utali wa kila kiasi kwamba hata baadhi ya nchi wanatumia kivutio vyetu vya Utalii kutangaza vipo kwai,hivyo ni jukumu la wataanzania na kwa kutumia vyombo vya habari kueleza kuhusu kivutio vyetu.
- “Tunajua Wizara ya Utalii inafanya kazi ya kutangaza Utalii wetu na vivutio vilivyopo lakini kwa kipindi hiki kila mmoja wetu kwa nafasi yake kutangaza utalii kwa wageni waliopo nchini kwetu,”amesema Waziri Mkuu. Na Said Mwishehe,Michuzi TV
Ad