ZANZIBAR IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU – RAIS DKT. SHEIN

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu, kutokana na misingi bora iliyowekwa na muasisi wa Taifa hili, marehemu Abeid Amani Karume.
  • Dk. Shein amesema hayo katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Mwembeshauri, ikiwa ni shamra shamra za maadhimiisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Alisema ukombozi uliofanywa na Chama cha ASP chini ya Uongozi thabiti wa marehemu mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964, umeweka misingi bora ya upatikanaji wa elimu nchini, na kubainisha kuwa itaondelea kutolewa bure katika awamu zijazo.

3-01

  • Alisema kabla ya Mapinduzi ya 1964, elimu ilitolewa kwa malipo, hivyo watoto wa wazalendo wa Zanzibar, hususan wanyonge walishindwa kupata fursa ya kusoma, sambamba na kutolewa kwa misingi ya ubaguzi kutegemea na kabila la mtu alikotoka.
  • Alisema kupitia Ilani ya uchaguzi wa ASP, marehemu Abeid Amani Karume alitangaza elimu kutolewa bure nchini kote, pale chama hicho kitakaposhinda na kukamata hatamu, jambo ambalo limeeendelea kutekelezwa hadi leo.

1-01

  • Dk. Shein alisema katika awamu tofauti za Uongozi, Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuendeleza sekta ya elimu kwa kuimarisha miundombinu ya elimu, ikiwemo ujenzi wa skuli hadi kufikia 381 hivi sasa kati yake skuli 284 zikiwa za Sekondari.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *