RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA DARAJA LA KIBONDE MZUNGU

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ujenzi wa barabara na daraja la Kibonde Mzungu ni uthibitisho wa Mapinduzi kwani kabla ya Mapinduzi hapakuwepo madaraja na barabara nzuri kama zinazojengwa hivi sasa hapa Zanzibar.

3-01

  • Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la Kibonde Mzungu, lililopewa jina “Daraja la Dk. Shein”, liliopo Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla iliyofanyika eneo hilo la Kibonde Mzungu ikiwa ni shamrashamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Aliongeza kuwa wakati huo daraja kubwa hapa Zanzibar lilikuwa ni daraja la Tingatinga lililopo Kaskazini Unguja ambalo halikuwa na sifa wala vigezo kama madaraja na barabara zinazojengwa hivi sasa ambazo zina ubora kwa wananchi kwa ajili ya usarifi wao na bidhaa zao.

 

2-01

  • Alisema kuwa baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 kila kitu kilishamiri zikiwemo barabara, nyumba na mambo mengineyo., “lakini hivi sasa tunachokitaka wenyewe tunajenga, na mimi nataka nikukumbusheni ujenzi wa daraja hili mara tu baada ya kulitembelea mnamo mwaka 2017 yalipotokea mafuriko na kuamuru kujengwa”.

1-01

  • Katika hafla hiyo, Rais Dk. Shein alieleza kwa ufupi historia ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kueleza juhudi zilizochukuliwa katika kuhakikisha wanyonge wa Zanzibar wanakuwa huru sambamba na kuimarika kwa sekta za maendeleo zikiwemo barabara.
  • Rais Dk. Shein alisema kuwa Mapinduzi yataendelea kusemwa kila siku kwani ni jambo ambalo lina maslahi ya wananchi wote licha ya kuwepo baadhi ya watu ambao hawapendi kuyataja, kuyazungumza wala kuyasikia.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *