RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA ZA KWAHANI JIJINI ZANZIBAR Matokeo ChanyA+ January 10, 2020 Taarifa Vyombo vya Habari, Taarifa ya Habari, Tanzania MpyA+, ZANZIBAR Acha maoni 999 Imeonekana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akitembelea Ujenzhi wa Nyumba mpya za Mji wa Kwahani Wilaya ya Magharibi Unguja ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mradi huo Kwahani Jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.Ndg.Khamis Mussa, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi huo unaofanyika katika eneo la kwahani RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika eneo hilo la ujenzi kwahani ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wananchi wa Kwahani, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Mji Mpya Kwahani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) Ad Share Facebook Twitter Stumbleupon LinkedIn Pinterest