WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WIKI MOJA KUREKEBISHWA KWA DOSARI KATIKA MACHINJIO YA MSALATO

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene hii  amegoma kufungua machinjio ya Msalato jijini Dodoma kwa kutokidhi vigezo vya ubora vinavyoridhisha ikiwemo ukarabati wa kiwango cha chini na kutoa muda wa wiki ya moja kurekebisha dosari zilizobainika.
  • Ametoa uamuzi huo wakati akitembelea jengo la machinjio ya Msalato jijini Dodoma wakati wa ziara aliyoifanya na kubaini kasoro mbalimbali zinazotakiwa kupatiwa ufumbuzi. “Sifungui hii machinjio kwa sababu hamjajiandaa na ujenzi uko hovyo kwahiyo siwezi kufungua kitu cha hovyo namna hii” Simbachawene alisisitiza.
A3-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiongea na Diwani wa Kata ya Msalato Mh. Ally Mohamed wakati wa ziara hiyo.
  • Akiongea katika ziara hiyo amesema amesikitishwa sana na ukarabati wa kurekebisha machinjio hayo kwani haukidhi viwango na ujenzi wake ni wa kiwango cha chini hivyo amemuagiza Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma Bwana Shabani Juma kuhakikisha ndani ya wiki ya moja kila kitu alichotolea maelekezo kifanyiwe marekebisho.
  • “Sijafurahishwa kwa kwakweli, majengo ya Serikali yanatakiwa kujengwa na mafundi classic, vitu vya Serikali viwe State of Art” Simbachawene alisisitiza.
  • Waziri Simbachene pia amegiza kuandaliwa kwa taarifa rasmi ya ukarabati huo ikiwa ni pamoja na thamani ya fedha zilizotumika katika zoezi zima la ukarabati na ujenzi wa  mifumo ya maji safi na maji taka.
A1 -01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene akipata maelekezo toka kwa Afisa Mipango miji wa jiji la Dodoma Bwana Shabani Juma wakati akikagua jengo la machinjio katika eneo la Msalato jijini Dodoma.
  • Naye Diwani wa Kata ya Msalato Mheshimwa. Ali Mohamed amesema kuwa amesikitishwa sana kwa kutofunguliwa kwa machinjio hiyo kwani wakazi wengi wa Kata yake wanategemea machinjio kwa shughuli zao za kila siku kwa sababu ni Wafugaji. Pia alisema Maelekezo yote yaliyotolewa na Mheshiwa Waziri Simbachawene wameyapokea na naamini kuwa yatarekebishwa kwa wakati.
  • Machinjio hiyo ya Msalato ilifungwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimazi wa Mazingira (NEMC) tarehe 31 Oktoba 2019 kutokana na sababu za mazingira yasiyokua safi na salama, kufuatia ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *