WAZIRI ZUNGU AWASILI MTUMBA NA KUSISITIZA UADILIFU

1-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikaribishwa rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Balozi Joseph Sokoine Naibu Katibu Mkuu.
  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amemtaka kila mtumishi katika Ofisi ya Makamu wa Rais atimize wajibu wake katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.
  • Hayo ameyasema hii leo mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma na kupokewa na Menejimenti na watumishi na Ofisi hiyo.
2-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo.
  • Akizungumza na watumishi wa Ofisi yake Waziri Zungu amewataka wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kuendelea kusimamia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
  • Ametoa rai kwa watanzania kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhifadhi na kusimamia Mazingira. “Simamieni Sheria bila kumuonea mtu, pale ambapo Sheria imekataza jambo simamieni Sheria na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka” Zungu alisisitiza.
3-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na sehemu ya watumishi wa Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo. Pamoja na mambo mengine amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo.
  • Awali aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambae sasa ni wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amekabidhi Ofisi rasmi kwa Waziri Zungu na kumtakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yake mapya.
  • “Tumefanikiwa katika katazo la mifuko ya plastiki, tumeridhia Mikataba na Itifaki mbalimbali na pia tuna program maalumu ya Upandaji mti nchi nzima ambayo ni endelevu” Simbachawene alisisitiza.
4-01
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ambae sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene akimkabidhi rasmi Ofisi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu. Makabidhiano hayo yamefanyika hii leo katika Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma.
  • Pia Waziri Simbachawene alisema kuwa mbali ya kufanikiwa katika kampeni ya katazo la mifuko ya plastiki lakini zaidi na elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi kuhusu tofauti ya vifungushio na vibebeo ambavyo bado wananchi wanachanganya.
  • Amempongeza na kumshukuru Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo kwa muda aliofanya nae kazi kwa ukaribu ambapo wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali yakiwemo kuridhia mikataba, itifaki na kanuni zinazohusu mazingira.
  • Waziri Zungu ameteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kushika nafasi hiyo baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo Mhe. Simbachawene aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *