WAFANYABIASHARA KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUZALISHA ZAIDI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wafanyabiashara wa ukanda wa Ziwa Victoria kuongeza uzalishaji wa bidhaa za samaki, matunda, nyama na mbogamboga ili kuwezesha uwepo wa safari za uhakika za ratiba kwa mashirika ya ndege kutoka nje ya nchi kupitia mkoa wa Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kufungua kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera na taasisi ambazo zinashughulika na usafirishaji mkoani Mwanza amesema uwepo wa ndege za ratiba unategemea idadi ya mizigo inayozalishwa katika ukanda huo.

Ad
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akifafanua wakati wa Mkutano wa siku moja uliowakutanisha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara kuweka mikakati endelevu ya usafirishaji wa minofu ya samaki wanaosafirisha nje ya nchi, jijini Mwanza.

“Mpaka sasa kuna mashirika mawili tu ya ndege yanayosafirisha mizigo ya samaki kupeleka nje ya nchi, idadi ya ndege hizo inaweza kuongezeka tu endapo mzigo unaozalishwa utaongezeka” alisema Waziri Mhandisi Kamwelwe.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa kwa sasa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) liko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kupata cheti kitakachoruhusu kusafirisha abiria na mizigo kwa nchi za (Europe hii kiswahili ni nn)

Kwa upande wake Waziri wa Mifupo na Uvuvi, Luhanga Mpina amewahakikishia wafanyabiashara kuwa yale ambayo yanaihusu Wizara hiyo wataanza kuyasimamia mara moja ili kuhakikisha mizigo yote inayotoka kwenye viwanda inasafirishwa kwa wakati na kuwafikia walaji.


Katibu Mkuu (Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho akiwaonesha Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kulia), eneo la kuwekea mizigo nje ya jengo la kuhifadhia mizigo wakati viongozi hao walipotembelea jengo hilo mizigo katika kiwanja cha ndege mkoani Mwanza.

Waziri Mpina ameongeza kuwa mpaka sasa kuna zaidi ya tani 200 za samaki ambazo huzalishwa kila siku kupitia viwanda vya Mwanza kuiomba Wizara kuhakikisha ratiba za ndege zinaongezeka ili kuwafanya wafanyabiashara kuzalisha zaidi.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemshukuru Waziri Mhandisi Kamwelwe kwa kuzikutanisha sekta zote ili kujadili na kuja na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha usafirishaji wa samaki unaendelea na kuwa na manufaa kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya Ziwa.

Waziri Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara kuwa wataendelea kusimamia ubora wa biadhaa hizo kwa kuboresha muonekano wa vifungashio ili uweze kulingana na mahitaji ya soko.


Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Bulayi, akifafanua jambo katika Mkutano wa siku moja uliowakutanisha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), WIzara ya Mifugo na Uvuvi, WIzara ya VIwanda na Biashara na wafanyabiashara wa minofu ya samaki wanaosafirisha nje ya nchi,jijini Mwanza.

Mashirika ya Ndege ya Rwanda na Ethiopia yalianza rasmi kusafirisha minofu ya samaki na mabondo tarehe 12 Mei 2020 ambapo mpaka sasa Shirika la Ndege la Rwanda limeshafanya safari mbili na Shirika la Ndege la Ethiopia limeshafanya safari moja na makampuni hayo kwa pamoja yameweza kusafirisha jumla ya tani 68.2

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *