UCHIMBAJI KINA CHA LANGO LA KUINGILIA MAJI KWENYE MITAMBO JNHPP WAKAMILIKA

Mhandisi Dismas Mbote

Ujenzi wa eneo la lango (Water Intake) la kuingilia maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme katika Mradi wa Julius Nyerere (Mw 2115) unatarajiwa kukamilika Februari 2022.

Mhandisi Dismas Mbote, msimamizi wa ujenzi wa njia za maji pamoja na Bwawa kwenye Mradi wa Julius Nyerere amesema utekelezaji wa njia hiyo ulianza Mwezi Oktoba 2019.

Ad
Mhandisi Dismas Mbote

Aliongeza kuwa kazi ya uchimbaji wa lango imekamilika kwa kuchimbwa kina cha mita 53 ambapo hivi sasa kazi inayoendelea ni uondoaji wa kifusi na uchimbaji wa mahandaki matatu yatakayotumika kupitisha maji.

“Vifusi ambavyo vinachimbwa katika mradi huu wa Julius Nyerere havitupwi, mawe yanasagwa na kuwa mchanga, kokoto na mawe mbalimbali ambayo hutumika kwenye ujenzi”, alisema Mhandisi Mbote.

Aidha, zitafanyika kazi za kuchoronga miamba pamoja na kuimarisha kuta kwa zege.

Maji yatakayo fua umeme kabla ya kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yataingia kwanza kwenye lango.

Pia kwa hivi sasa imeletwa mashine ya kuchoronga miamba ambayo ni ya kwanza kwa Tanzania na inayotarajiwa kuongeza kasi katika uchimbaji wa mahandaki ya kupeleka maji kwenye mitambo.

Handaki la kwanza litakuwa na urefu wa mita 350, la pili mita 410 na la tano mita 570 hadi kwenye mitambo ya kufua umeme.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

3 Maoni

  1. Hello there, just became alert to your blog through Google, and found that
    it’s truly informative. I’m gonna watch out for
    brussels. I will be grateful if you continue this in future.
    A lot of people will be benefited from your writing. Cheers!

    Najlepsze escape roomy

  2. I was examining some of your articles on this website
    and I conceive this site is rattling informative!
    Keep putting up.?

  3. Hi, I do think this is an excellent web site. I stumbledupon it 😉 I am going to come back once again since i have book-marked it. Money and freedom is the greatest way to change, may you be rich and continue to guide other people.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *