RAIS MAGUFULI AWASHUKURU VIONGOZI WA DINI NA WATANZANIA KWA MAOMBI DHIDI YA CORONA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati alipokuwa akiendesha Harambee ya Papo kwa papo kwa ajili ya upanuzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 7 Juni 2020. Katika Harambee hiyo jumla ya Shilingi Milioni 17 zilipatikana pamoja na mifuko 76 ya Saruji na Mhe. Rais Magufuli alichanga peke yake kiasi cha Shilingi Milioni 10.

Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo tarehe 07 Juni, 2020 alipokaribishwa kuwasalimu Waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Chamwino Mkoani Dodoma baada ya kuhudhuria Misa Takatifu ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Paulo Mapalala.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watumishi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Ikulu mara baada ya Misa ya Jumapili ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu.

Rais Magufuli amesema Mwenyezi Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake ni kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yamepungua, na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi za uzalishaji mali, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ugonjwa huo ungesababisha madhara makubwa.

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Paulo Mapalala akishukuru mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuendesha Harambee iliyofanikisha kupatikana kiasi cha ya Shilingi Milioni 17 pamoja na mifuko 76 ya Saruji.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza ugonjwa huo ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliye muweza wa yote. Akiwa Kanisani hapo Mhe. Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha shilingi 17,229,000/- (ikiwemo shilingi Milioni 10 aliyochangia yeye mwenyewe)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Paulo Mapalala mara baada ya misa ya Jumapili ya Sikukuu ya Utatu Mtakatifu katika Kanisa hilo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *