SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA TAIFA WAUENDESHAJI WA SHUGHULI ZA UTALII NCHINI TANZANIA WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Wadau wa Sekta ya Utalii na Waandishi wa Habari leo jijini Arusha wakati wa Uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA.

Serikali imezindua rasmi mwongozo wa uendeshaji wa Shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la Corona na kuwataka wadau sekta hiyo kuzingatia matakwa yaliyo katika mwongozo huo ili kulinda usalama wa Watanzania na watalii wanaowasili nchini kutembelea vivutio vilivyopo.

Akizindua mwongozo huo leo jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka wadau wote wa Sekta watimize wajibu wao kwa kuhakikisha wageni wote wanaoingia nchini wanakuwa salama na wanaondoka salama pasipo kuambukizwa au kuambukiza wengine virusi vya Corona.

Ad
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakiangalia kurasa na maudhui ya  Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA baada ya kuuzindua rasmi leo jijini Arusha.

Dkt. Kigwangalla amesema Serikali imeamua kuzindua rasmi mwongozo huo ili kuilinda Sekta ya Utalii pamoja na afya za wadau wote wanaohusika na sekta hiyo na kuongeza kuwa hatua hiyo itaongeza na kujenga imani ya wageni wanaoitembelea Tanzania kutokana na masharti ya kiafya yaliyoainishwa katika mwongozo huo ambayo watoa huduma za utalii wanatakiwa kuyazingatia.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Katikati), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu (wan ne kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda (wa Pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Aloyce Nzuki, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi na Viongozi wa Vyama vya Mawakala wa Utoaji wa huduma za Utalii nchini Tanzania wakionesha  Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini Arusha.

Ameongeza kuwa mwongozo huo huo utaisaidia biashara  ya Utalii kuanza upya wakati huu wa janga la CORONA ambapo Tanzania imeamua kufuangua  mipaka yake kufuatia baadhi ya nchi zikiwemo za Ulaya kuanza kufungua anga kwa  kuruhusu  mashirika makubwa ya ndege kuanzisha safari za ndege za abiria kutua  katika nchi hizo kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Wadau wa Sekta ya Utalii wakifuatilia tukio la Uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA

 Amebainisha kuwa Tanzania imeondoa masharti mengi ambayo yalikuwa yakikwamisha watalii wengi kuja nchini Tanzania likiwemo lile la mtalii kukaa Karantini kwa muda wa siku 14.

Dkt. Kigwangalla amewahakikishia wageni mbalimbali wanaopanga safari zao kuja nchini Tanzania waje bila hofu yoyote kwa kuwa Tanzania ni nchi salama.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *