BODI YA WAKURUGENZI YA IMF IMEIDHINISHA LEO DOLA ZA MAREKANI MILIONI 14.3 ZA MSAMAHA WA KODI WA MADENI TULIYOKUWA NAYO – RAIS MAGUFULI

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeidhinisha dola za marekani milioni 14.3 za msamahaa wa kodi za madeni.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Jengo la Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mjini Dodoma.

Ad

“Leo ninapozungumza tumepata fedha za msahama, Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha leo dola za marekani milioni 14.3 za msamaha wa kodi wa madeni tuliyokuwa nayo na kwasababu tulipambana vizuri sana na ugonjwa wa corona” – amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa msamahaa huo umekuja wakati muafaka, na kwamba atamwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa IMF kwa niaba ya watanzania kwa lengo la kuwapongeza kwa kutambua juhudi za Tanzania.

Amesema fedha hizo pia zitatumika katika kuendelea kupambana na corona na kushugulikia katika maeneo mengine ambayo yatasaidia kumaliza tatizo la corona nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KENYA DKT. WILLIAM SAMOEI RUTO, NAIROBI NCHINI KENYA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.