TTCL YASAINI MKATABA WA ZAIDI YA SH. BILIONI TANO

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameliagiza Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL) kubuni teknolojia ya gharama nafuu itakayowawezesha kuyafikia maeneo kiuchumi.

Ad


Kamwelwe ameyasema  hayo baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini wa kupeleka mawasiliano vijijini kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kata 32 kwa vijiji 45 kwa wakazi wapatao 521,897 kwa gharama ya sh. Bilioni 5.1.


Waziri Kamwelwe alisema mradi huo ni wa awamu ya tano  kwa maeneo ya mipakani na kanda maalum  ambapo awamu hii inatumia vyanzo vya ndani vya fefha  na kufanikisha kutumiza idadi ya kata 987 kwa jumla ya kata 955 kutoka kwenye awaku 10 za awali. 

Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba wakibadilishana hati mara baada ya kusaini mkataba katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


“Hatua  ya kusaini mkataba huu nia kujivua kwa serikali  na wadau wote hada watoa huduma za mawasiliano  ambapo mpaka sasa serikali  kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote  imetekeleza miradi 10.


Amesema utekelezaji wa jumla wa mpango wa upelekaji huduma ya mawasiliano katika maeneo yenye mawasiliano hafifu ambayo mengi yapo vijijini. 


Mhandisi Kamwelwe amesema  kwa kushirikiana na kampuni za simu itaweza kufanikisha upelekajiwa mawasiliano kwa kata 987 kabla ya mwaka 2021 kumalizika. 


“Tanzania ni wakati muafaka kuitumia TEHAMA kimkakati na kuona namna ambavyo inaweza kutuletea mabadiliko chanya ya maisha yetu  bila kujali sehemu tunapoishi, “alisema. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa utiaji wa saini ya mkataba kati ya  Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) katika Hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Akijibu changamoto zilizopo mpaka wa Rwanda na Kenya, Mhandisi Kamwelwe alisema leo anatarajia kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Profesa Palamagamba Kabudi kwa ajili ya kuangalia namna ya kuzitatua. 


Changamoto hizo wamekuwa wakikutana nazo wamiliki wa malori nchini pindi wanaposafirisha mizigo yao na hii ni kutokana na ugonjwa wa Corona. 

Hatua hiyo imekuja siku moja,  baada ya Wamiliki wa Malori Nchini(TATOA) kuzungumzia changamoto wanazokutana nazo maeneo ya mipaka hiyo na kuiomba serikali kuwasaidia kutokana na gharama wanazokutana nazo. 


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote,Justina Mashiba alisema mfuko hadi sasa umeshatekeleza miradi 302.
Amesema jumla ya sh.  Bilioni 60 zilitokewa kama ruzuku kwa TTCL kupeleka mawasiliano vijijin na kuongeza kuwa  hadi sasa mfuko umetenga ruzuku ya sh. Milioni 150.9 kwa ajili ya mradi huo. 
Hata hivyo alisema mawasililiano ndio chachu ya maendeleo hivyo husaidia ukuaji wa uzalishaji wa viwanda.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *