WAZIRI ZUNGU: MAPATO YA MFUKO WA MAZINGIRA YAAINISHWE KWENYE SHERIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema ipo haja ya kuanisha vyanzo vya mapato ya mfuko wa mazingira kwenye sheria ili kuongeza wigo katika usimamizi wa mazingira.

Zungu amesema hayo leo alipokutana na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ofisini kwake jijini Dodoma.

Ad
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma leo.

Alisema kwa kuanisha kazi hizo kwenye sheria kutasaidia kuwafanya wananchi wawe sehemu ya kuboresha na kuhifadhi mazingira badala ya kuachia Serikali peke yake.

Waziri Zungu aliongeza kuwa alipendekeza kuwepo kwa na chanzo cha mapato yanayotokana na uchafuzi kupitia vyombo vya moto kwa kuwa hivi sasa upo utaratibu wa kutoza ada mara moja na magari hayo hurudi barabarani kuchafua mazingira.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ofisini kwake jijini Dodoma leo.

“Magari haya yanatumika miaka 10 yanakuja nchini mwetu kutumika tena yanatozwa excise duty mara moja lakini likiingia mitaani linaanza tena kuchafua, tukasema kila mwaka yapewe cheti ya kuonesha yanafanyiwa ukarabati na kuingia tena barabarani,” alisema.

Zungu alifafanua kuwa kazi za mfuko wa mazingira zisiwe tu kufanya warsha na mikutano ambayo haigusi uhalisia hivyo maeneo ya mfuko yafanyiwe kazi hasa kwenye uchafuzi wa mazingira, hewa ya ukaa, ukataji wa miti.

Wadau wa mazingira kutoka Jukwaa la Kilimo Tanzania pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu ofisini kwake jijini Dodoma leo. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *