Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kama uivyoonekana pichani.

RAIS MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA RELI YA KATI (SGR) SEHEMU YA DAR ES SALAAM – MOROGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la Reli nchiniTRC kabla ya kuondoka katika stesheni hiyo ya Soga mkoani Pwani.

Rais Dkt. John Magufuli tarehe 28 Juni, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kwa sehemu ya kwanza ya Dar es Salaam – Morogoro na kuelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Rais Magufuli amesafiri kwa gari kandokando ya reli hiyo kuanzia Kisarawe hado Soga Mkoani Pwani na kisha akapanda kiberenge kilichopita katika reli hiyo mpya kuanzia Soga hadi Kikongo kabla ya kuendelea na safari yake kwa gari kuelekea Morogoro.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kuhusu mradi wa Reli ya Kisasa wa Standard Gauge kuanza LOT 1 kipande cha Dar -Moro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo ndani ya Behewa la Treni ya Uhandisi wakati alipokuwa akielekea Mlandizi mkoani Pwani ambapo amekagua kazi za ujenzi wa kipande cha Reli ya Kisasa kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro ambapo ujenzi umefikia asililimia 80.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kazi ya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya reli hiyo imefikia asilimia 82 ambapo Watanzania 13,000 wamenufaika na ajira na inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu (2020).

Akizungumza na wananchi wa Soga na Kikongo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa kupata mradi huo na ametaka waendelee kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kunufaika zaidi na mradi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuhutubia Wananchi wa Kisarawe Mkoani Pwani ambapo alizindua mradi mkubwa wa Maji-Picha na Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isaack Kamwelwe pamoja na Mtendaji Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Reli.

Aidha, Rais Magufuli amesikiliza kero za wananchi hao ambapo ameendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa Shule ya Msingi Soga na kufanikiwa kukusanya shilingi 68,535,000/- zikiwemo shilingi Milioni 5 alizochangia yeye mwenyewe, na amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kufika Kijijini hapo ili kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mmiliki wa shamba kubwa lililopo kijijini hapo ambalo halilimwi.

Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa kuhakikisha anatatua tatizo la maji linalokikabili kijiji cha Soga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye treni ya Uhandisi mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa Reli ya Kisasa wa Standard Gauge kuanza LOT 1 kipande cha Dar -Moro katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani
Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kama uivyoonekana pichani.
Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kama uivyoonekana pichani.

Ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imechukua hatua madhubuti za kutekeleza mradi huo ambao utagharimu shilingi Trilioni 7.02 kwa sehemu ya kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora Mkoani Dodoma, pamoja na kutekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa megawati 2,115 za umeme katika Bwawa la Nyerere ili kukuza uchumi wa Watanzania na kuinua kipato cha wananchi na hivyo amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizo.

Akiwa Mlandizi, Rais Magufuli amesikiliza kero za wananchi na kumuagiza Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso kuhakikisha Wizara ya Maji inatatua tatizo la maji la Mitaa ya Mbwawa Shule na Mbwawa Mkoleni na pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara ya lami ya Mafia – Mzenga – Vikumbulu ili kuunganisha Mlandizi na reli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufika eneo la Mlandizi mkoani Pwani wakati akikagua kipande cha Reli kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro ambapo ujenzi wake umefikia asililimia 80.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mlandizi mkoani Pwani wakati alipotoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro ambapo ujenzi umefikia asililimia 80.

Rais Magufuli amewasili Mjini Morogoro na kesho ataendelea na ziara yake Mkoani hapa ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mahandaki ya reli ya kisasa (standard gauge) sehemu ya Morogoro – Makutupora, kuzindua barabara ya lami ya Rudewa – Kilosa na atafanya mkutano wa hadhara katika eneo Mkadage Wilayani Kilosa. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu (2020) huku wakikumbuka kudumisha amani, umoja na mshikamano pamoja na kuwachagua viongozi watakaowafaa

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *