RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHANDAKI YATAKAYOPITISHA TRENI YA KISASA YA UMEME (SGR) KILOSA MKOANI MOROGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Eng. Isack Kamwelwe pamoja na viongozi mbalimbali akiweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Mahandaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mahandaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Umeme Standard Gauge katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Eng. Isack Kamwelwe pamoja na viongozi mbalimbali akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya Rudewa-Kilosa Km 24 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi ya Mawaziri, wakuu wa Mikoa, viongozi mbalimbali, akikata utepe ili kuzindua mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mawaziri, baadhi ya Viongozi wa Serikali, katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni zinazojenga mradi wa Reli ya Kisasa SGR Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye handaki la Reli ya Kisasa ya SGR lenye urefu wa Km 1.1 ambalo litapitisha treni hiyo katika eneo la milima ya Kilosa mkoani Morogoro.
Sehemu ya Handaki kubwa lenye urefu wa Kilometa 1.1 ambalo litapitisha treni hiyo katika eneo la milima ya Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita ndani ya Handaki kubwa lenye urefu wa kilometa 1.1 kulikagua mara baada ya kuweka jiwe la msingi la miradi hiyo ya ujenzi Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akitoka kwenye Handaki kubwa la Reli ya Kisasa mara baada ya kulikagua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kuweka kumbukumbu kwenye ukuta wa Handaki kubwa mara baada ya kumaliza kulikagua Handaki hilo mkoani Kilosa mkoani Morogoro
Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga zaidi ya shilingi bilioni 250 katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi katika Halmashauri zote 184 nchini

Taarifa hii imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *