KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MBIONI KUANZA JIJINI DODOMA

Na Tito Mselem Dodoma,

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, amefanya ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu ( Refinery)   cha Eyes Of Africa Ltd kilichopo katika eneo la Area D pembezoni mwa Uwanja wa Ndege wa Jiji la Dodoma.

Ad

Ziara hiyo yenye lengo la kukagua hatua za ujenzi uliofikiwa na kiwanda hicho ambacho ni kiwanda cha kwanza nchini cha kusafisha madini ya dhahabu na fetha.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kushoto) akipewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar.

Kiwanda cha Eye Of Africa kinachomilkiwa na Ferenc Molnar ambaye ni raia wa Yugoslavia ni miongoni mwa kampuni nne zilizopewa leseni ya usafishaji wa madini ya dhahabu (Gold Refinery Licence) hapa nchini, kampuni nyingine ni pamoja na STAMICO-Mwanza, Geita Gold Refinery na African Ayes-Geita.

Katika ukaguzi huo, Prof. Msanjila aliambatana na Kamishina Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani, Bertha Luzabiko ambopo walifurahishwa na hatua iliyofikiwa na kampuni hiyo.

Prof. Msanjila amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Eye Of Africa Ferenc Molnar kuandika barua kwa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinisha mambo muhimu yanayotakiwa ili serikali isaidie katika kufanikisha mahitaji ya Kampuni hiyo.

Aidha, Prof. Msanjila, ameiahidi kampuni hiyo, kuhakisha inapata wateja kutoka sehemu mbalimbali hususan wachimbaji wadogo mara kampuni hiyo itakapo anza uzalishaji.

Pia, Prof. Msanjila amesema, mara baada ya viwanda vya usafishaji madini ya dhahabu kuanza kazi, Serikali itasitisha usafirishaji wa dhahabu ghafi kwenda kusafishwa nje ya nchi na badala yake madini ghafi yote yatasafishiwa nchini kabla hayajasafirishwa kwenda nje ya nchi.

Wakati huo huo, Prof. Msanjila amempongeza Molnar kwa hatua nzuri aliyoifika ikiwemo ufungwaji wa mashine mbalimbali za kusafisha madini ya dhahabu katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake, Mkrugenzi Mtendaji wa Eye Of Afrika Ferenc Molnar, amesema mara baada ya kuanza kwa uzalisha kampuni yake itakuwa na uwezo wa kuzalisha kilo 40 za dhahabu kwa siku na itamtoza mteja asilimia 0.5 ya gharama ya mzigo utakaosafishwa kiwandani hapo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Oni moja

  1. You have observed very interesting details!
    ps nice site.Leadership

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *