RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU WA WILAYA, MKURUGENZI NA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA 2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1 na Mkurugenzi Mtendaji 1, kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Ad

Kabla ya uteuzi huo, ACP Advera John Bulimba alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA na anachukua nafasi Bw. Godfrey William Ngupula.

Pili, Rais Magufuli amemteua Bw. Solomon Isack Shati kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Solomon Isack Shati alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi na anachukua nafasi ya Bw. Bryceson Paul Kibasa.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kept (Mst) George Huruma Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya 2, kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Bw. Omary Mwanga kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Bw. Omary Mwanga anachukua nafasi ya Bi. Husna Juma Sekiboko.

Pili, amemteua Bw. Saitoti Zelothe Stephen kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Saitoti Zelothe Stephen alikuwa Afisa Tarafa Wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara na anachukua nafasi ya Bw. Hassan M. Mkwawa.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza tarehe 09 Julai, 2020.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *