JKT YATANGAZA MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO MWAKA 2020

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara  waliochagulwa  kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2020 .

Akizungumza leo Julai 16, 2020 Makao Makuu ya Jeshi  hilo Wilayani Chamwino  Mkoani  Dodoma,  Mkuu wa Tawi la Utawala, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Julius  Kadawi amesema kuwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles  Mbuge anawakaribisha    waliochaguliwa  kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha , utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa kupitia mafunzo hayo.

Ad

“Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz”, Alisisitiza Kanali Kadawi

Aidha, Kanali Kadawi amesema kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai, 2020 ambapo mafunzo yatafunguliwa rasmi Agosti 1, 2020.

Akifafanua, Kanali Kadawi amesema kuwa kwa upande wa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa  macho  (Physical disabilities) wanatakiwa kuripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa  jamii hiyo.

“Kutokana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID -19) nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama ilivyoelekezwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya zitazingatiwa kwa kipindi chote vijana watakapokuwa katika mafunzo”, Alisisitiza Kanali Kadawi

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi  za JKT Rwamkoma- Mara, JKT Msange- Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga- Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba- Tanga, JKT  Makuyuni- Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, JKT Mtabila- Kigoma, JKT Itaka- Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa- Rukwa, JKT Nachingwea- Lindi,JKT Kibiti na Oljoro- Arusha.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *