RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA RC, KM, NKM NA DC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jumanne Fhika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Ad

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Fhika alikuwa Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Bw. Christopher Ole Sendeka.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Nzuki alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Sanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Prof. Kitila Alexander Mkumbo.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Dkt. Allan Kijazi anachukua nafasi ya Dkt. Aloyce Nzuki aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, na pia Dkt. Allan Kijazi ataendelea kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Nadhifa Kemikimba alikuwa Mkurugenzi katika Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Mhandisi Anthony Sanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Fadhili Mohamed Juma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mkoani Geita.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Fadhili Mohamed Juma alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi na anachukua nafasi ya Josephat Paulo Maganga ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

Bw. Josephat Paulo Maganga anachukua nafasi ya Bw. Patrobas Katambi.

Wateule wote wawepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *