TUNADI SERA ZETU NA WANANCHI WAWEZE KUTUPIMA KUTOKANA NA SERA ZETU – RAIS MAGUFULI

“Tanzania tunatakiwa tuijenge, Tanzania ya Nyerere inatakiwa iende hivi na mimi niwaombe, niwaombe sana ndugu zangu wanasiasa wezangu kama ambavyo imekuwa kawaida yenu katika uchaguzi huu uwe uchaguzi maalum”

“Tufanye kampeni zetu kwa upole, tufanye kampeni zetu kwa kumtanguliza Mungu, tufanye kampeni zetu kwa kujua sisi ni taifa la Tanzania, tufanye kampeni zetu kwa kujenga umoja wa Taifa letu Tanzania”

Ad

“Tunadi sera zetu na wananchi waweze kutupima kutokana na sera zetu wasitupime kwa matusi tunayo tukanana mimi naamini tukiende hivyo uchaguzi huu utakuwa mzuri sana, uchaguzi huu utakuwa huru sana”

Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

“Na ni wahakikishie viongozi wa siasa mimi ni mwezenu tunajenga nyumba moja na nyumba hiyo tunayoijenga ni Tanzania nataka kuwathibitishia nitatoa ushirikiano mzuri sana kwa vyama vyote ili twende na maadili yetu kama ambavyo tulifundishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarange Nyerere”

“Tanzania tunaitaji maendelea zaidi, Tanzania tunahitaji kwenda mbele zaidi , kwahiyo nawashukuru sana kwa ninyi mliwakilishwa kuja hapa nimeona kuna vyama vingi sana katika vyama hakuna chama kidogo sisi wote tuko sawa sawa”

“Na niviombe kwasababu nina amini vyama vyote vitaendesha kampeni kiustaarabu basi tukawe wavumilivu lakini niviombe vyombo vya kusimamia haki ikiwepo vyombo vyetu vya dola tuvumilie kidogo tusitumie nguvu mahali ambapo hapahitajiki kutumia nguvu”

“Lakini niwaombe na nyinyi wanasiasa msiwachokoze walinda amani msiwafanye wakatumia nguvu pahali ambapo nyinyi mnataka watumie nguvu kwahiyo sisi sote vyama vyote”

“Mimi nina uwakika tukimtanguliza Mungu katika kampeni zetu tutafanya kampeni nzuri na sasa uwanja uko huru Mhe. Jaji (Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Semistocles Kaijage) ameshaeleza hapa, ameshatangaza ratiba huu ndio wakati wa kujinadi, huu ndio wakati wa kupiga maneno ya siasa baada ya hapo yule akayeshinda tunaanza kazi siasa zinabaki bungeni na kwenye halmashauri za wilaya’

“kwahiyo kwa sasa hivi ni ruksa kadri ya ratiba itakavyokuwa imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kila mmoja akafanye kampeni zake kwa uhuru, uwazi akahubiri vizuri”

“Na bahati nzuri hata Mungu ametusikia maombi yetu kwasababu Mungu ni mkubwa ukimuomba anafanya corona imepotea imekimbia ina koromea pahali pengine tumeishinda corona hii ni kwa maajabu ya Mungu tulimuomba Mungu kwa siku tatu madhehebu yote tukamshukuru pia kwa siku tatu lakini kila mmoja kwa wakati wake wamekuwa wakimtanguliza Mungu katika kuliweka Taifa hili”

“Nataka niwahakikishie ndugu zangu ushindi huu wa corona kukimbia si nguvu zetu ni nguvu za yule aliyeko juu amesikiliza kilio chetu kwahiyo tuendelee kumshukuru Mungu na ndio maana uchaguzi huu utafanyika kwa amani hapa pote tupo salama”

“Na mimi napenda sana tumshukuru mwenyezi Mungu kwa huruma na upendo mkubwa alioutoa kwa Taifa letu ndugu zangu kama nilivyosema mwaka huu ni mwaka wa chaguzi, uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani”

“Uchaguzi ni zoezi muhimu hivyo basi napenda kutumia fursa hii kuwasihii sana Tume kusimamia vizuri, uchaguzi huu kwa kufata katiba, sheria na taratibu za uchaguzi za nchi yetu”


“Narudia kuviimiza vyama vya siasa kushiriki kwenye uchaguzi huu na kujiepusha na vitendo vya vurugu, vurugu hazijengi, vurugu zinabomoa
na niviombe vyombo vya ulinzi na usalama visimamie usalama wa Watanzania yule atakaye chokoza kwa kufanya vurugu basi atakuwa amechokoza yeye lakini mimi nina imani kubwa kwamba mambo yote yataenda vizuri”

“Napenda pia kuwahimiza wananchi kujiandaa kushiriki kwenye uchaguzi huo kwanza kwa kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa ili kusikiliza sera lakini pia kwenye zoezi la upigaji kura kama nilivyosikia kampeni za uchaguzi zitafunguliwa tarehe 26 Agosti 2020 na zitakamilika tarehe 27 Oktoba 2020 na uchaguzi utafanyika tarehe 28 Oktoba 2020 nafikiri itakuwa siku ya jumatano kwahiyo siku ya uchaguzi itakuwa siku ya mapumziko tutaitangaza rasmi.” – Rais Dkt. John Magufuli, Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Njedengwa Dodoma

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BI JAMIE COOPER

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bi. Jamie …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.