NGOs ZAKUMBUSHWA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Na Mwandishi Wetu Iringa

Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imeyataka Mashirika hayo kuwasilisha taarifa za kila robo mwaka zinazoonesha fedha na kazi wanazozifanya kwa Msajili ili aweze kujua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yalipo Mashirika hayo.

Ad

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya msajili wa NGOs Grace Mbwilo wakati wa ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa na Mashirikia Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Iringa.

Grace amesema kuwa Serikali inafarijika  kuona Mashirika yanashirikiana nao kufanya kazi za kusaidia jamii na kutekelza miradi mbalimbali katika maeneo waliopo kwa kufuata taratibu na vipaumbele vilivyoqekwa na Serikali katika eneo husika.

Baadhi ya miradi inayotekelezwa na shirika la IOP Mkoani Iringa ikiwemo ukarabati wa madarasa mawili katika shule za msingi Kisoliwaya na Ilula na ujenzi wa madarasa kwa lengo la kupunguza msongamano katika shule ya msingi Ilula.

Ameongeza kuwa Mashirika yanapopata fedha nyingi kutoka kwa wafadhili ili kutekeleza miradi mbalimbali ila  wanatakiwa kuhakikisha wananchi waliokusudiwa wananufaika na miradi hiyo.

“Mwongozo tuliouzindua hivi karibuni unasisitiza uwazi na uwajibikaji kwasababu tunajua fedha mnaomba kwa ajili ya watanzania hivyo ni wajibu wa Serikali na Jamii husika kufahamu zinafanya nini za zimeleta matokeo gani” alisisitiza

Aidha Mkurugenzi huyo Msaidizi amebainisha kuwa kwa sasa NGOs na Serikali zinashirikiana hivyo ameyasihi Mashirika kutotumia njia za mkato kwani watachelewa kufanya kazi zao hivyo kukwamisha kutekeleza miradi iliyokusudiwa kwa wakati.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Jaina Said amesisitiza Mashirika kufuata sheria na taratibu zilizopo kwa kutochelewesha taarifa muhimu zinazohitajika kuwasilisha na Mashirika hayo katika Ofisi ya Msajili na kusubiri faini.

“Wengine wanaona faini ni hela ndogo, tunakupiga faini kukumbusha wajibu wako, lakini ikiwa ni zaidi ya mara moja tunakuangalia vizuri kama unafaa” alisema Jaina.

Hata hivyo timu hiyo imelipongeza shirika la Ilula Orphanage Program (IOP) kwa miradi yenye lengo la kusaidia jamii hasa katika kusomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Akilezea utekelezaji wa Miradi ya Shirika Ilula Orphanage Program (IOP) Katibu Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Edson Msigwa amesema kuwa Shirika lake linafanya shughuli mbalimbali za kusaidia jamii ikiwemo kulea na kusomesha watoto, kujenga madarasa na kuwezesha wananchi kiuchumi.

“Shirika letu lina miradi zaidi ya 20 na kubwa tunajishughulisha na kusomesha watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na tayari watoto 2000 wamenufaika na mradi huo” alifafanua.

Nayye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Ilula Bi. Joyce Michael amelishukuru Shirika Ilula Orphanage Program (IOP) kwa kukarabati madarasa mawili Shuleni hapo hivyo kupunguza msongamano wa wanafunzi ambao ungeweza kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

#LIVEDAY2: JUKWAA LA KODI NA UWEKEZAJI 2024

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.