KAMPUNI YA ANDOYA YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA UMEME

Jiwe la msingi la Kampuni ya Andoya liliwekwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Mtandazi, wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,alipofanya ziara ya kukagua shughuli za kuzalisha Umeme katika kampuni hiyo, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma, Agosti 01, 2020.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, ameitaka Kampuni ya Andoya inayozalisha Umeme kwa kutumia Maporomoko ya Maji ya Mto Mtandazi kutanua wigo wa Kampuni hiyo ili kuongeza uzalishaji zaidi.

Masanja alisema hayo, Agosti 01, 2020, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma,wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo ili kuona shughuli za kufua na kuzalisha Umeme wa Megawati moja kwa kutumia Maporomoko ya Maji ya Mto Mtandazi zinazofanywa na kampuni hiyo tangu mwaka 2015.

Ad
Moja ya Nguzo za umeme zinazotumika kusambaza umeme unaozalishwa na Kampuni ya Andoya kwa wakazi wa vijiji vitatu vilivyo karibu na mradi huo.

Alisema kampuni ya Andoya inazalisha umeme ambao huliuzia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na pia katika Vijiji vitatu vilivyokaribu na mradi huo ambavyo ni Lifakara, Kilimani na Mbangamao.

Masanja aliueleza Uongozi wa Andoya kuwa wana uwezo na nafasi kubwa ya kuweza kutanua mradi huo na kuongeza uzalishaji wa Umeme kwakuwa eneo la mradi ni kubwa na linatosha.

“Kampuni yenu inanafasi kubwa ya kukuwa kiuzalishaji,sababu mnachanzo cha uhakika ambacho kina maji ya kutosha na yanayopatikana muda wote, azma ya Serikali ni kuwa na uwezo wa kuzalisha MWA 10,000 ifikapo 2025. hivyo, mchango wa wazalishaji wadogo unahitajika sana”, alisema Mhandisi Masanja.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, (kulia) akipata maelezo katika eneo la Bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Mtandazi ya kampuni ya Andoya kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Alex Andoya(kushoto), alipofanya ziara ya kukagua shughuli za kuzalisha Umeme katika kampuni hiyo, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma, Agosti 01, 2020.Wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme, Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga na wapili kulia na Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, Janeth Andoya.

Aidha alizitaka Taasisi za kifedha kuendelea kushirikiana na kuwaunga mkono wazalishaji binafsi wa umeme nchini kwa kuwapatia mikopo pale inapohitajika kwa lengo la kujenga, kuboresha au kutanua wigo wa mradi husika kwa kwakuwa miradi hiyo inadumu kwa muda mrefu.

Aliwasihi wasimamizi wa mradi huo waendelee kuusimamia vizuri ili uendelee kuzalisha umeme kwa kuwa miradi ya kuzalisha umeme wa maji ikisimamiwa vizuri huishi  na kudumu kwa muda mrefu.

Meneja wa kituo cha kuzalisha umeme cha Andoya,Jasper Bubelwa ,akimpa maelezo ya uzalishaji wa umeme katika kampuni hiyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,(wa pili kulia) alipofanya ziara ya kukagua shughuli za kuzalisha Umeme kwa kutumia maporomoko ya Maji ya Mto Mtandazi, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma, Agosti 01, 2020.

Vilevile aliwaagiza wasimamizi husika wa mradi huo kubadilisha Mita za umeme zinazotumiwa na wateja wao katika vijiji vitatu vilivyo karibu na mradi huo ambazo ni za mfumo wa kizamani zinazomruhuru mteja kutumia kwanza huduma ya umeme ndipo alipie, badala yake wawafungie mita za LUKU zinazotumika sasa ambazo mteja hulipia umeme kadri anavyotumia.

Aliendelea kusisitiza kuwa jukumu la Serikali ni kupitia Wizara ya Nishati ni kutunga Sera na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika Sekta ya Nishati. Kwa muktadha huo, Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake itaendelea kusimamia sheria, taratibu na kanuni za uwekezaji katika sekta ya Nishati ili kuendelea kuvutia wawekezaji nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Andoya, Alex  Andoya aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Nishati na Taasisi ziliochini yake kwa ushirikiano walioutoa kwa kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.

Aina ya mita zinazotumiwa na wateja wa Umeme wa Andoya katika vijiji vitatu vilivyokaribu na mradi huo ambazo zinamruhusu mteja kutumia huduma ya umeme kabla ya kulipia.

Na Zuena Msuya, Ruvuma

Aidha aliahidi kushirikiana na taasisi za kifedha kuongeza uzalishaji wa umeme katika mradi wao kama alivyoshauriwa kwa kuwa wanachanzo cha uhakika cha kuzalisha umeme.

Aidha alieleza kwa ufupi juu ya mradi huo, kwa kueleza kuwa  Ujenzi wa Mradi wa Andoya ulibuniwa na Marehemu Baba yake Mzee Mbunda Andoya ambapo ulijengwa kwa awamu mbili (2), ya kwanza ilihusu ujenzi wa mtambo wa kuzalisha MW 0.5 ambapo ujenzi ulianza mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2015.

Awamu ya pili ilihusisha uwekaji wa mtambo wa MW 0.5 ambapo ulikamilika mwaka 2018  na kuwa na jumla ya mitambo yenye kuzalisha MW 1.0.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *