MAENEO YANAYOTENGWA KWA UWEKEZAJI YAPIMWE -NAIBU WAZIRI MABULA

Na Munir Shemweta, WANMM BUKOMBE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameziagiza idara za ardhi kwenye halmashauri kuhakikisha maeneo yanayotengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji yanapimwa  sambamba na kuwa na mpango wa matumizi bora ardhi katika vijiji.

Ad

Dkt Mabula alisema hayo jana wilayani Bukombe akiwa katika ziara yake ya kikazi kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na kukagua miradi inayejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mkoa wa Geita.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Chato Hati ya Ardhi alipokuwa katika ziara ya kikazi kwenye mkoa wa Geita jana.

Alisema , kuna baadhi ya maeneo kwenye halmashauri nchini yametengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji lakini hayajapimwa huku baadhi ya vijiji vikiwa havijawekewa hata mipango ya  matumizi bora ya ardhi jambo alilolieleza linaweza kuwakimbiza wawekezaji na kuleta migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wakati wa mchakato wa kutenga maeneo ya uwekezaji  ndani ya halmashauri, ni vizuri utengaji maeneo hayo ukaenda sambamba na kuyapima maeneo hayo huku juhudi zikiongezwa kuviwekea vijiji mipango ya matumizi bora ya ardhi.

‘’Asije muwekezaji ndiyo muanze zoezi la uhaulishaji, ni vizuri kuyapima maeneo hayo ya uwekezaji kwa kuwa suala la uhaulishaji linaweza kuchukua muda na linataka idhini ya Rais ‘’ alisema Dkt Mabula

Viongozi na Watendaji wa sekta ya ardhi wilayani Chato wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Geita jana.

Naibu Waziri wa Ardhi ambaye katika ziara yake hiyo alitembelea pia halmashauri za wilaya za Chato na Geita na kuziagiza halmashauri kuongeza kasi katika uwekeji mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji sambamba na kuvipatia vyeti ili kuondokana na migogoro ya mara kwa mara hasa ile ya wakulima na wafugaji.

Katika taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita ilieleza kuwa imeandaa na kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji vitano vya Kagwe, Kidete, Bukombe, Ilalwe na Nasihukulu kwa kushirikiana na Timu ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi Taifa.

Akigeukia utendaji kazi wa ofisi za ardhi za mikoa zilizozinduliwa hivi karibuni, Dkt Mabula alizitaka halmashauri kuzitumia ofisi hizo katika shughuli mbalimbali za masuala ya ardhi hata pale ambapo kuna upungufu wa watumishi pamoja na ukosefu wa vifaa.

Alisema, halmashauri  kushindwa kuzitumia ofisi za ardhi za mikoa katika masuala mbalimbali ya ardhi kama vile upimaji haitakuwa na maana ya kuzianzisha ofisi hizo ambazo jukumu lake kubwa ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *