KAMPUNI YA GGML NA HALMASHAURI YA MJI WA GEITA WAMESAINI MAKUBALIANO YA MPANGO WA KUSAIDIA JAMII WENYE THAMANI YA SH BIL 9.2

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson (kulia) akikabidhi mkataba wa makubaliano Mpango wa uwajibika kwa jamii mwaka huu (CSR) kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto)
Mkuu wa Sheria kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited (GGML), David Nzaligo na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Richard Jordinson wakisaini makubaliano hayo.
Baadhi ya maofisa kutoka kampuni ya GGML na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita wakisaini makubaliano hayo huku wakishuhudiwa na baadhi ya maofisa wengine.

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) pamoja na Halmashauri ya Mji wa Geita mapema jana imesaini makubaliano ya utekelezaji wa Mpango wa kusaidia Jamii (CSR) kwa mwaka 2020 wenye thamani ya Sh bilioni 9.2.

Makubaliano hayo yamethibitisha ahadi GGML kwa Serikali baada ya kutekeleza mabadiliko yaliyomo kwenye kifungu cha 105 cha Sheria ya Madini ambacho kinajumuisha utekelezaji wa Mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Ad

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *