MILLIONI 715 ZATUMIKA KUBORESHA OFISI, MAKAZI YA VIONGOZI TANGA

Shilingi milioni 715 zimetumika kukarabati Nyumba za Wakuu wa Wilaya za Lushoto na Korogwe, kujenga nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto na Ofisi nane za tarafa katika Wilaya hizo.

Ujenzi na Ukarabati wa nyumba na ofisi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa azima  Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha mazingira ya kazi kwa viongozi nchini.

Hayo yamebainika wakati wa makabidhiano ya Nyumba na Ofisi hizo katika Wilaya za Lushoto na Korogwe mkoani Tanga kati ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Mabughai na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary (wa pili kushoto) wakionesha hati ya makabidhiano ya Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai.

Akikabidhi majengo hayo yaliyojengwa na kukarabatiwa na  Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema  makazi na Ofisi bora ni chachu kwa viongozi  kufanya kazi kwa bidii.

Dkt. Jingu amesema  Chuo cha Maendeelo ya Jmaii na Ufundi Mabughai kimejikita zaidi katika kuhakikisha kinaleta tija na kutoa mchango wake katika  maendeleo na kuongeza ufanisi na  hivyo, wataendelea kushirikiana na wadau mablimbali katika kutekeleza miradi mbalimbali.

“Niseme tu muda si mrefu tutaanzisha Kampuni ya Ujenzi kama ilivyo Suma JKT ili tuongezee nguvu zaidi ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kiwango kikubwa zaidi” alisema

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za  kuboresha makazi na Ofisi za viongozi ili kuweka mazingira mazuri ya uwajibikaji wa viongozi hao katika kuwahudumia wananchi wao.

Ad
Muonekano wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mara baada ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha Ofisi na mkazi ya viongozi.

“ Rais John Pombe Magufuli amedhamiria kuboresha mazingira ya makazi na Ofisi za viongozi ili tuweze kumsaidia kutatua changamoto zainazowakabili wananchi” alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika amekishukuru Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai kwa kukarabati nyumba yake kawa kikwango cha juu.

“Nasema huu si ukarabati bali wamejenga upya kwani kila kitu kimebadilika ukiangalia picha za zamami utasema imejengwa na sio kukarabati” alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kisa Gwakisa amekiri ukarabati wa nyumba hiyo umekidhi viwango na kuwapongeza kuwa Chuo cha Mabughai kwa kazi nzuri na kuahidi kuendelea kushirikiana nacho katika kutekeleza miradi mingine Wilayani humo.

“Nakiri nimeridhika na ukarabati huu ukipita nje ya nyumba hii utadhani hoteli ya kitalii vile kumbe  ni nyumba ya Mkuu wa Wilaya inaopendeza sana” alisema

Awali akitoa maelezo ya miradi ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi na Nyumba za Viongozi mkoani Tanga uliofanywa na Chuo  Mabughai, Mkuu wa Chuo hicho Aidan Felix amesema  Chuo kimeshirikisha jamii kwa karibu katika kutekeleza miradi hiyo kwa kutumia mafundi na wataalam kutoka katika maeneo husuka hivyo kuifanya miradi hiyo kuwa ya wananchi.

Ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Lushoto umegharimu zaidi ya shilingi milioni sitini na mbili, nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe zaidi ya shilingi million 106, na ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto umegharimu zaidi ya shilingi million 231 na ofisi nane za tarafa zimegharimu Millioni 315.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *