CHUO CHA MADINI KUWA SEHEMU YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Picha ya pamoja ya kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nzega (kushoto), VIongozi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (katikati) na wafanyakazi wa Wizara ya Madini (kulia) wakisikiliza wakati wa hafla ya kukabidhi Chuo cha Madini (MRI) kulelewa na UDSM katika hafla iliyofanyika Agosti 19, 2020 Kampasi ya Nzega.

Imethibitishwa kuwa sasa Chuo cha Madini kilichokuwa chini ya Wizara ya Madini kitakuwa sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.

Hayo yalithibitishwa Agosti 19, 2020 wakati wa Hafla ya Kukabidhi Chuo hicho Kampasi ya Dodoma na Nzega Kulelewa kwa muda na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam  katika hafla iliyofanyika katika Kampasi ya Nzega  Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora .

Ad

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema  kuwa Tukio Hilo ni moja ya hatua za uboreshaji wa Sekta ya Madini pamoja na kuhakikisha nchi ya Tanzania  inazalisha wataalam wa kutosha  na wenye ujuzi wa hali ya juu katika sekta ya madini kuanzia ngazi ya Astashahada hadi Stashahada ili nchi iweze kusimamia rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia bila kutegemea wataalam kutoka nje.

Alisisitiza kuwa, Serikali  inaamini kuwa,  ulezi wa Chuo  cha Madini kama ilivyoelezwa kwenye mchakato wa awali, kitaendelea  kutoa mafunzo ya mchundo na mafundi sanifu katika sekta ya Madini lengo  likiwa  kukifanya kitengamae hatimaye kiweze kujiendesha.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akieleza jambo katika hafla ya kukabidhi Chuo cha Madini (MRI) kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika Agosti 19, 2020 Kampasi ya Nzega. (Kushoto) ni Prof. William Anangiye Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es salaam.

Asteria Muhozya na Steven Nyamiti, Nzega

“Uleaji utakaotolewa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ulenge kukiimarisha Chuo Cha Madini Kitaaluma, kuboresha miundombinu na kuongeza ufanisi  wa utendaji kazi,” Alisisitiza Nyongo.

Aliongeza kuwa, Mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na UDSM yasilenge kuondoa majukumu ya msingi ya Chuo Cha Madini.

“Ni matarajio ya Serikali na Wizara kuwa  Chuo hiki kitafikia viwango vya Kitaaluma vinavyokubaliwa Kitaifa na Kimataifa,” alisema Nyongo.

Akielezea kwamba,  kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kutokuwepo kwa Sheria ya kuanzishwa Chuo Cha Madini; uvamizi  wa maeneo hususan KampasiI ya Nzega na kuongeza kwamba  anaamini  changamoto hizo zitatuliwa chini ya ulezi huo na kwamba , hafla hiyo  ni matokeo ya utatuzi wa changamoto hizo.

Pia, alizungumzia  hatua mbalimbali ambazo zimechukukiwa  na Serikali, ambazo zimepelekea Sekta ya Madini sasa imeanza kukua kwa kasi kubwa, ambapo Mwaka 2019 iliongoza kwa Ukuaji  kwa asilimia 17.7.

Alisema kutokana na jitihada hizi sasa  mapato yanayotokana na madini yameongezeka  ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 zilikusanywa Shilingi Bilioni 346 kutoka Shilingi Bilioni 194  Mwaka 2016/17, kwenye Mwaka 2019/2020 zlikusanywa zaidi ya Shilingi Bilioni 470 ambalo  ndiyo lilikuwa lengo la Wizara.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *