RAIS MAGUFULI AZINDUA KANISA NA AFANYA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI CHAMWINO, DODOMA

Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya aliposhiririki Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” na kuzindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Rais Dkt. John Magufuli amezindua Kanisa, nyumba ya Mapadre na Groto katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino iliyopo Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

Katika uzinduzi huo, Rais Magufuli ameambatana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya ambaye amelibariki Kanisa, Groto na nyumba ya Mapadre na baadaye kuongoza Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ndani ya Kanisa hilo.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru baada ya kukabidhi michango kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya aliposhiririki iliyotokana na harambee kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Ujenzi wa Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino, Groto na ukarabati wa nyumba ya Mapadre wa Kanisa hilo ulianza tarehe 08 Juni, 2020 siku moja baada ya Rais Magufuli kuhudhuria Ibada ya Fumbo la Utatu Mtakatifu na kisha kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo ambapo pamoja nae, Waumini wa Kanisa hilo na Madhehebu mbalimbali ya Kikristo na Kiislamu wamejitokeza kuchangia na kufanikiwa kukamilisha ujenzi huo.

Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima amemshukuru Rais Magufuli kwa upendo na uamuzi wake wa kufanya ujenzi mkubwa wa Kanisa, Groto na kukarabati nyumba ya Mapadre wa Parokia hiyo ambayo kwa kuwa kwake Ikulu Chamwino ina historia ya kuwahudumia Marais wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha harambee kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Baba Askofu Mkuu Kinyaiya amemshukuru Rais Magufuli kwa kuongoza kazi kubwa iliyofanyika kuiboresha Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino na amemuelezea kuwa ni kiongozi mwenye uthubutu na anayejali watu anaowaongoza.

Katika Ibada hiyo, Baba Askofu Mkuu Kinyaiya amembariki na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuliongoza Taifa vizuri na hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, na pia amewataka Watanzania wote kushiriki uchaguzi mkuu huku wakidumisha amani na mshikamano, na kuhakikisha wanachagua viongozi wacha Mungu, wanaotafuta uongozi kwa njia za amani, wanaojiamini na wasiotoa rushwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea michango kutoka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Chamwino baada ya kuitisha Harambee aliposhiririki Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Katika salamu zake, Rais Magufuli amemshukuru Baba Askofu Mkuu Kinyaiya kwa kuongoza Misa Takatifu na kulibariki Kanisa, Groto na Nyumba ya Mapadre, na pia amewashukuru wote waliojitokeza kuchangia ujenzi na ukarabati huo ambao umefanyika kwa mafanikio makubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi michango kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya aliposhiririki iliyotokana na harambee kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na umoja wa Watanzania ulioneshwa katika ujenzi huo ambapo waliojenga na waliochangia fedha wametoka katika Madhehebu mbalimbali ya Dini.

Akiwa anatoa salamu hizo, Rais Magufuli ameamua kuendesha harambee nyingine ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Waislamu wa Chamwino ambapo amefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Milioni 48, mifuko 48 ya saruji na tripu 5 za mchanga kutoka kwa Waumini wa Parokia ya Bikira Maria Imakulata na Waumini wa Madhehebu mengine mbalimbali waliojitokeza papo hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua msikiti wa Chamwino na maemneo yake baada ya kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wake wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” wakati wa uzinduzi wa Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania )TEC) Padri Dkt. Charles Kitima na Paroko wa Kanisa hilo Paul Mapalala baada ya kushiriki Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki na waumini wengine katika Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *