TAASISI YA MOYO (JKCI) YAPOKEA MASHINE YA KUPIMA UMEME WA MOYO

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) mara baada ya kumkabidhi msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) kwa msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo kwa watoto Dkt. Sulende Khuboja akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha Mafunzo na Utafiti Dkt. Naiz Majani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito (Fetal Cardiograph). Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta watoto wanaotibiwa Jkci kliniki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza madhara ya mafuta mwilini wagonjwa waliokuwa wanasubiri kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram – ECHO) na Umeme wa moyo (Electrocardiogram – ECG) wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yapokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) yenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka kwa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *