NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP)

Mafundi wakiendelea na kazi ya kukamilisha lango la handaki la kuchepusha maji ya mto wakati wa kujenga Bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la mto Rufiji wa Julius Nyerere. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, Agosti 22, 2020.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,amekagua  ujenzi wa Mradi wa Bwawa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2115 kwa kutumia Maporomoko ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere( JNHPP).

Mhandisi Masanja amefanya ukaguzi huo hususani katika eneo la Bwawa la Maji ili kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi, Agosti 22, 2020.

Ad
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja(kushoto) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa handaki la kuchepusha maji kutoka kwa Mhandisi Mkazi ambaye pia ni mshauri wa mradi huo, Mhandisi Mushubila Kamuhabwa( kulia), wakati wa ziara ya Naibu katibu mkuu huyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la mto Rufiji wa Julius Nyerere, Agosti 22,2020 mkoani Morogoro.

Mhandisi Masanja alitembelea maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa mradi huo likiwemo Handaki la kuchepusha Maji ya Mto, Handaki la kupeleka Maji katika mitambo ya kufua Umeme, pamoja sehemu itakapojengwa jengo maalum la kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme(Controlroom).

Vilevile alikagua mitambo ya kusaga na kuchakata kokoto, pia na mitambo ya kuchanganya Zege ambayo inatumika katika shughuli za ujenzi katika eneo la mradi ikiwemo bwawa husika.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja (kushoto) akipata maelezo ya ufanyaji kazi wa mitambo ya kuchanganya zege kutoka kwa Mhandisi mkazi na Mshauri wa mradi huo, Mhandisi Mushubila Kamuhabwa( kulia), wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la mto Rufiji wa Julius Nyerere, Agosti 22,2020 mkoani Morogoro.

Ikumbukwe kwamba Kazi ya ujenzi wa mradi huo ilianza rasmi mwezi Juni 15, 2019 ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 36,  na unatarajiwa kukamilika mwezi  June 2022, chini ya  Mkandarasi wa ubia wa Kampuni Arab contractors na Kampuni El Sewedy.

Mradi wa JNHPP umeiwezesha na kuitambulisha Tanzania kuingia katika ulingo wa Kidunia na kushika nafasi ya 70 kwa kujenga Bwawa kubwa la kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji kati ya mabwawa yote ya aina hiyo duniani.

Muonekano wa mitambo ya kuchanganya zege itakayotumika wakati wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, Agosti 22,2020 mkoani Morogoro.
Sehemu itakayowekwa Mikanda ya kusafirisha Zege kutoka mitamboni ya kuchanga Zege hadi kwenye bwawa la kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere wakati wa ujenzi wa bwawa hilo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Agosti 22,2020 mkoani Morogoro.

Vilevile umeiwezesha kushika nafasi ya nne kwa nchi za Afrika ambapo la kwanza ni Renaissance lililopo Ethiopia linalozalisha (Megawati 6450), la pili ni Mambila nchini Nigeria (Megawati 3050), la tatu ni Kakula Kabako nchini Angola (Megawati 2170.

Na katika Ukanda wa Afrika Mashariki linashika nafasi ya kwanza,likifuatiwa na Kaborabasa la Msumbiji linalozalisha megawati 1,245, Kafue Gorge nchini  Zambia litakalokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati  1,145 pindi litakapokamilika mwaka 2024, na  Karuma nchini Uganda linalozalisha megawati 600.

Ukamilishwaji wa ujenzi wa Mahandaki matatu ya kupeleka maji ya kuzungusha mitambo ya kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere,ukiendelea wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Agosti 22,2020 mkoani Morogoro.

Na Zuena Msuya, Morogoro

N.B: Tafadhali soma Jarida la Wizara ya Nishati, linalotoka kila mwisho wa mwezi ili kupata habari motomoto kwa kina zaidi zinazohusu sekta ya Nishati na Taasisi zilizochini yake, pia linapatikana katika tovuti ya wizara ambayo ni www.nishati.go.tz.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja(katikati) akitazama shughuli za ujenzi zinazoendelea katika mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Agosti 22,2020 mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Mhandisi Mkazi na mshauri wa mradi huo Mhandisi Mushubila Kamuhabwa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *