ALAT YAZITAKA HALMASHAURI KUHESHIMU FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT) Elirehema Kaaya amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinatumika kikamilifu ikiwa ni pamona na kubana mianya yote ya ubadhirifu inayoweza kujitokeza.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa katika halmashauri mbalimbali nchini ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuona Tanzania nzima inakuwa yenye maendeleo.

Ad

Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi shule, zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyopo katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ,alisema ni vyema halmashauri zinazotekeleza miradi mbalimbali chini, kuhakikisha zinazingatia suala la matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa hatua ambayo mbali na mambo mengine itawezesha miradi mingine kuendelea kujengwa.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa sasa ipo kazini kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakuwa yenye tija, ili kufanikisha hilo inatakiwa kuwe na nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha za ujenzi wa miradi ili malengo yote yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa” alisema Kaaya.

Alisema halmashauri hizo hususani zilizopo katika miji, zina kila sababu ya kuhakikisha zinafanya matumizi bora ya adhi kwa kujenga majengo hayo ya ghorofa kwa kuwa kutazifanya halmashauri hizo kuwa na majengo bora na mengi katika eneo dogo.

Katibu Mkuu huyo wa ALAT pia alisema halmashauri zote zinazotekeleza ujenzi wa miradi yake kwa kuzingatia utaratibu huo wa matumizi bora ya ardhi sambamba na thamani ya fedha katika miradi yake mbalimbali, zinaunga kwa vitendo harakati za Rais John Magufuli kulieletea Taifa maendeleo.

Aliipongeza Manispaa ya Ilala kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa shule uliozingatia matumizi bora ya ardhi sambamba na fedha iliyoendana na miradi hiyo jambo lililoiwezesha kupata hati safi.

“Huu ni mfano mzuri wa matumizi ya fedha hizi za Serikali, lakini pamoja na hili imekuwa moja ya manispa bora nchini ambazo zimekuwa zikipata hati safi, hili ni jambo linaloonyesha kuwa ina nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi hiyo” alisema Kaaya.

Alimaliza kwa kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha inatumia mashine za kielektroniki (POS) katika utoaji huduma ili kurahisisha kazi ya ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya Serikali.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *