WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI AMTAKA MKANDARASI UJENZI DARAJA LA MAGUFULI JIJINI MWANZA KUTOA AJIRA ZA VIBARUA KWA WAZAWA

Muonekano wa sasa wa Daraja la Kigongo-Busisi, lenye urefu wa wa mita 3200, na barabara unganishi (km1.66). Daraja hili linagharamiwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa asilimia 100.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amemtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Magufuli  jijini Mwanza, kutoa ajira nyingi za vibarua kwa vijana wazawa ili wanufaike na mradi huo.

Agizo hilo amelitoa Waziri huyo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo yaliyofikiwa had sasa.

Ad
Mhandisi Mshauri Abdulikarim  Majuto, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Mhandisi Dkt. Leonard  Chamuriho, wakati Waziri huyo alipotembelea Ujenzi wa Daraja la kigongo-busisi,  jijini  Mwanza.

“Miradi yote ambayo tunalipa pesa zetu wenyewe tuhakikishe wakandarasi wazawa wanajumuishwa kwenye kazi, ili kuweza kupata uzoefu kwa vijana wetu wa kitanzania”.amesisisitiza waziri chamuriho

Waziri Chamuriho pia amewataka Bodi ya Wakandarasi nchini (CRB), kuhakikisha inawaongezea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kuwa pamoja katika Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa barabara, na madaraja.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Mhandisi Dkt. Leonarad Chamuriho, akikagua Ujenzi wa Daraja la Magufuli, lijulikanalo kama daraja la Kigongo-Busisi lenye mita 3200 na barabara unganishi (km1.66)

”Katika miradi yote mikubwa lazima tuweke asilimia kubwa kwa wakandarasi wazawa ili tuweze kupata wakandarasi wenye weledi”.aliongezea waziri chamuriho

Aidha, Waziri Chamuriho amewapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa daraja hilo na kumuagiza mkandarasi wa daraja hilo kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa wa Mwanza ,Mhandisi Fedestus Malibe, amesema kuwa Daraja la JPM linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara kuu ya Isagara-sengerema-Geita- katika ziwa Victoria na litakapokamilika litarahisisha usafirishaji baina ya pande zote mbili. 

Naye, Afisa Utumishi wa kampuni ya CCE onesphory Ngonyani, amemhakikishia Waziri huyo kuendelea kutoa ajira kwa vijana wazawa wa eneo hilo, hadi pale ujenzi huo utakapokamilika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *