Serikali imesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa jiji la dodoma kwa kiwango cha lami ya njia nne yenye urefu wa kilometa 112.3 ili kupunguza msongamano katika jiji hilo mikataba iliyosainiwa ni baina ya Wakala wa Barabara
(TANROADS) kwa niaba ya Serikali na wakandarasi wawili Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na AVIC INTL Project Engineering Company walioshinda zabuni ambao watajenga barabara hiyo kwa kipindi cha miezi 36. Mkandarasi Civil Engineering Construction Corporation
(CCECC), atajenga kilometa 52.3 kuanzia Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port na mkandarsi AVIC INTL Project Engineering Company atajenga kilometa 60 itakayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu hadi Nala.