Na Farida Ramadhani, Dar es Salaam
Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimeshauriwa kuunganisha nguvu zao kupambana na changamoto ya utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa makundi ya kigaidi zinazotishia usalama na kuharibu uchumi wa nchi hizo .
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mwenyekiti wa Maafisa Wandamizi wa HAZINA wa SADC, Bw. Doto James wakati akifungua Kikao cha Maafisa Waandamizi (Makatibu Wakuu) wa HAZINA na Benki Kuu wa nchi wanachama wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho, Bw. James ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho kitakachofanyika kwa siku mbili, alisema kuwa changamoto hiyo imesababisha baadhi ya nchi wanachama kuingia katika orodha ya nchi zilizo kwenye athari ya kuingia kwenye vikwazo vya kimataifa kwa kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya Kikosi cha Masuala ya Fedha (Financial Action Task Force), hali iyonaweza kuathiri malengo ya jumuiya ya kuvutia uwekezaji.
Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo na nyingine kadhaa za kijamii, kimazingira na kiuchumi Jumuiya hiyo imeendelea kutekeleza azma yake ya kufikia malengo ya maendeleo iliyojipangia kupitia Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa SADC hali inayoashiria kuwa Jumuiya hiyo ni imara kutokana na kuwepo kwa sera nzuri na mifumo mizuri wa kitaasisi ndani ya Jumuiya hiyo.
“Pamoja na mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana kwa miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi wanachama zimeendelea kukabiliana na changamoto nyingine katika sekta za uchumi ikiwemo ukuaji mdogo wa uchumi, kuongezeka kwa nakisi ya bajeti na hii changamoto mpya ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona”, alisema.
Bw. James alisema katika kikao hicho Makatibu Wakuu hao watajadili na kutoa mapendekezo ya ajenda mbalimbali za masuala ya fedha na uwekezaji kwenye nchi za SADC ikiwemo athari za Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 yatakayowasilishwa kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu wa SADC utakaofanyika tarehe 15 Julai, 2020
Alisema kuwa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji, pamoja na mambo mengine, wanajukumu la kusimamia itifaki ya Fedha na Uwekezaji katika Jumuiya ya SADC kwa lengo la kuhakikisha Sera na Maamuzi ya Baraza la Mawaziri wa SADC kwenye masuala yanaohusu Fedha na Uwekezaji vinatekelezwa.
“Ili kukabiliana na athari hizo, ni vema nchi wanachama kutumia mifumo ya kitaasisi katika kutafuta njia mbadala zenye ubunifu ili kuharakisha hatua za kuimarisha uchumi ndani ya jumuiya yetu, ni matumaini yangu kuwa kikao hiki ni njia muafaka katika kujadili changamoto za kiuchumi na kutoa mapendekezo ya kitaalam yatakayowasilishwa katika Mikutano ya Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu kama ilivyoanishwa katika agenda za mikutano hiyo”, alisema Bw. James.
Alizitaja ajenda nyingine watakazo jadili na kutoa mapendekezo kuwa ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano uliopita wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji uliofanyika Windhoek, Namibia mwezi Julai 2019, kupokea na kujadili taarifa ya hatua iliyofikiwa ya namna uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda wa SADC (SADC Regional Development Fund) na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maandalizi ya Miradi ya Maendeleo wa SADC (Project Preparation Development Facility).
Viongozi hao pia watajadili na kupata taarifa ya hatua iliyofikiwa katika uanzishaji wa Mfuko Maalum wa Kugharamia Miradi ya Muundombinu ya Usafirishaji wa Nishati ya Umeme (Regional Transmission Infrastructure Financing Facility – RTIFF) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, kupitia taarifa ya maendeleo ya Sekta ya Fedha ya Magavana wa Benki Kuu nakupitia taarifa ya utekelezaji wa masuala ya udhibiti wa fedha haramu.
Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu wa SADC unaondaliwa katika kikao hicho ulipangwa ufanyike kuanzia tarehe 13 hadi 17 Julai, 2020 lakini kutokana na mlipuko wa COVID-19, mkutano huu utafanyika kwa njia ya mtandao kama ilivyoelekezwa katika Mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika tarehe 18 Machi 2020, Dar es Salaam.
Kevin De Bruyne https://manchester-city.kevin-de-bruyne-ar.com is a name every football fan knows today.
Football in Saudi Arabia https://al-hilal.saud-abdulhamid-ar.com is gaining more and more popularity and recognition on the international stage, and Saud Abdul Hamid, the young and talented defender of Al Hilal, is a shining example of this success.
Казахский национальный технический университет https://satbayev.university им. К.Сатпаева
Kylie Jenner https://kylie-cosmetics.kylie-jenner-ar.com is an American model, media personality, and businesswoman, born on August 10, 1997 in Los Angeles, California.
Brazilian footballer Ricardo Escarson https://orlando-city.kaka-ar.com dos Santos Leite, better known as Kaka, is one of the most famous and successful players in football history.
Liverpool https://england.liverpool-ar.com holds a special place in the history of football in England.
When Taylor Swift https://shake-it-off.taylor-swift-ar.com released “Shake It Off” in 2014, she had no idea how much the song would impact her life and music career.
The Formula One World Championship https://world-circuit-racing-championship.formula-1-ar.com, known as the Formula Championship in motor racing, is the highest tier of professional motor racing.
Michael Jordan https://chicago-bulls.michael-jordan-ar.com is one of the greatest basketball players of all time, whose career with the Chicago Bulls is legendary.
Muhammad Ali https://american-boxer.muhammad-ali-ar.com is perhaps one of the most famous and greatest athletes in the history of boxing.
Manny Pacquiao https://filipino-boxer.manny-pacquiao-ar.com is one of the most prominent boxers in the history of the sport.
The road to the Premier League https://english-championship.premier-league-ar.com begins long before a team gets promoted to the English Premier League for the first time