WAKULIMA MBINGU KILOMBERO WANUFAIKA NA UWEZESHAJI WA KILIMO CHA KOKOA

Na Mwandishi Ifakara

Wakulima wa zao la Kokoa Mbingu Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamenufaika na uwezeshaji kutoka Shirika la Africa WildLife lililowezesha kuongeza thamani ya zao la Kokoa kutoka kuandaa miche mpaka uzalishaji.

Ad

Hayo yamebainishwa na wanufaika hao wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini unaofanywa na Ofisi ya Msajili wa NGOs.

Mtaalamu wa masuala ya Kilimo kutoka Shirika la Africa WildLife Alexander Mpwaga (kulia) akielezea namna Shirika hilo lilivyowawezesha Chama cha Wanaolima Kokoa MOCO-AMCOS kupata nyenzo za kisasa za kuhifadhi na kukausha Kokoa wakati wa zoezi la Ofisi ya Msajili wa NGOs kutembelea Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo lililopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. Wa kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanaolima Kokoa MOCO-AMCOS Rashem Mrembe na wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Charles Mpaka.

Akizungumza namna walivyonufaikia na Shirika hilo Mwenyekiti wa Chama cha Wanaolima Cocoa MOCO-AMCOS Rashem Mrembe amesema kuwa hapo nyuma kumekuwa na tatizo la kukausha zao la Kokoa kutokana na kuwepo kwa mvua nyingi hivyo Shirika la Africa WildLife limewasaidia kupata teknolojia ya kukausha bila nishati ya jua.

Ameongeza kuwa, mara baada ya kupata tekinolojia hiyo wamefanikiwa kuongeza thamani na bei nzuri ya kuuza.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanaolima Kokoa MOCO-AMCOS Rashem Mrembe akionesha jinsi ya kupata mbegu zinazotokana na zao hilo wakati wa zoezi la Ofisi ya Msajili wa NGOs kutembelea Miradi inayotekelezwa na Shirika la Africa WildLife lililopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Charles Mpaka.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuweka mazingira rafiki kwa Mashirika haya kufanya kazi zao kwani inatusaidia kupata msaada na uwezo zaidi wa kufanya shughuli zetu” alisema

Naye mzalishai wa miche ya Mikokoa Neema Mlagile amelishukuru Shirika la African WildLife kwa kuwapa elimu iliyowasaidia kujua kuwa zao hilo lina fursa ya kupata kipato kikubwa kinachowezesha kujikwamua kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Charles Mpaka (wa pili kushoto) akizungumza na uongozi wa Shirika la Africa WildLife lililopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro wakati wa zoezi la Ofisi ya Msajili wa NGOs kutembelea Miradi inayotekelezwa na NGOs nchini. Wa tatu kushoto ni Meneja Programu wa Shirika hilo Pastor Majingi na kulia ni Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili Dereck Mwanjombe.

Aidha Mtaalamu wa masuala ya Kilimo kutoka Shirika la Africa WildLife Alexander Mpwaga amesema Shirika lao linaendelea kutoa elimu na misaada ya kimiundombinu kwa wakulima katika Mkoa wa Morogoro ili kuhakikisha wakulima wananufaikia na kilimo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Charles Mpaka amelipongeza Shirika la Africa WildLife kwa kuwasaidia wakulima kuwapatia Teknolojia rahisi ili kuongeza thamani za mazao yao kwa kupata soko la uhakika litakalowasaidia kupata kipato kitakachowakwamua kiuchumi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *