Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakuru ametembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda cha cha kusindika maziwa na kusindika vyakula vya mifugo cha Kahama Fresh Ltd kinachojegwa kata kihanga wilayani Karagwe pia shamba la mfano mahindi na eneo la ufugaji wa ng’ombe, mbuzi pamoja na kondoo lililopo eneo la kikurura wilaya ya karagwe. Januari 04, 2021.
Dkt. Bashiru amepongeza jitihada za mwekezaji mzawa wa Kahama Fresh Limited, Bw. Jossam Ntangeki kwa kusaidia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na dira Serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda pia kuzalisha ajira ambapo mpaka sasa kampuni ya imetoa ajira 130 kwa vijana wa kitanzania na kiwanda kitakapoanza uzalishaji zitatolewa ajira Zaidi ya 200.
Dkt. Bashiru ameelezwa changamoto anazozipata mwekezaji ambazo ni kukatika kwa umeme kila mara unaosababisha baadhi ya kazi kukwama na hadi sasa huduma ya TANESCO haipo kabisa takribani siku 30 pia kukosa kwa umeme katika eneo la ufugaji kikurula ambapo inasababisha kushindwa kutumia mashine za kukamua maziwa.
Dkt. Bashiru amemaliza kwa kumtoa hofu mwekezaji huku akiwasiliana na Waziri wa Nishati Dkt. Kalemani ili kutatua tatizo la kukatika kwa umeme katika eneo la ujenzi wa kiwanda na kuleta umeme katika eneo la ufugaji, nae Dkt. Kalemani amemuhakikishia mwekezaji kutatua changamoto hizo mara moja pia atafika eneo la uwekezaji ifikapo mwezi Februali 05, 2021
Nae, Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Limited, Jossam Ntangeki wakati akitoa taarifa ya kiwanda kwa Dkt. Bashiru amesema kuwa kiwanda kitakuwa na uwezo wa kusindika lita 10,000 kwa siku ambapo lita 5,000 zitazalishwa na mashamba ya ufugaji ya Kahama Fresh Ltd na lita 5,000 zitazalishwa na wafugaji walioko maeneo jirani na uwekezaji huo unategemea kukamilika ifikapo mwezi June 2021.