Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo Ashinda Pambano la Masumbwi Birmingham Uingereza

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo (miaka 23) jumapili tarehe 08 Septemba 2018 alimshinda kwa TKO (Technical KnockOut) bondia Muingereza Sam Eggington bondia (miaka 25)

Mwakinyo ambaye katika pambano hilo hakuwa anapewa nafasi ya kushinda, alionyesha umahiri wa hali ya juu na kulimaliza pambano katika round ya pili tu.

Ad

Bondia huyo Mtanzania ambaye alipewa taarifa za kupambana na bondia Eggington majuma mawili tu kabla ya tarehe ya pambano hilo ambalo lilikuwa ni moja ya mapambano yaliyopangwa kuwa ya utangulizi kabla ya mpambano uliosubiriwa na dunia kati ya bondia Muingereza Amir Khan na Samuel Vagras ambapo Khan alishinda kwa pointi.

Pambano hilo ambalo halikuwa la kuwania ubingwa wowote lilifanyika mjini Birmingham katika uringo maarufu duniani uitwao Birmingham Arena

Tazama pambano zima Kwema kubofya link hii

https://youtu.be/jWQiF3Dppzc

#SisiNiTanzaniaMpyA+

#MATAGA

Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SHONZA: WAZAZI NDIYO WALEZI WA KWANZA WA MTOTO

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *