CHAMWINO: “Kaitumie sheria inayokupa mamlaka ya kuwafikisha mahakisha mahakamani wala rushwa ‘DIRECT’ bila kupita kwa yeyote” – RAIS MAGUFULI

Viongozi walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, wamekula kiapo mbele yake katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma siku ya Jumatano Septemba 12, 2018.

“Nenda ukafanye kazi.” Kauli ya Rais Magufuli akimuagiza Mkurugenzi wa mpya wa Taasisi ya Kusuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP Diwani Athimani Msuya mara baada ya kumwapisha.

Katika maagizo yake, Mhe. Rais alisema; “Na kikubwa kabisa mimi ningependa ukatumie sheria.. ambayo mnayo.. ambayo huwa inawapeleka wala rushwa direct badala ya kupitia kwa DPP. Kwa sababu saa zingine huwa kuna mabishano kati ya DPP na TAKUKURU.. nani ampeleke nani.. na panakuwa na ucheleweshwaji saa nyingine wa kupelekwa wala rushwa kwenye Haki. Unakuta mla rushwa ameshikwa redhanded lakini hafikishwi mahakamani; Nataka ukalishughulikie hili.” alisisitiza Rais Magufuli

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.