Serikali itaunda tume ya uchunguzi itakayohusisha timu ya wataalamu na vyombo ya dola, kuhakikisha chanzo cha ajali kinatambulika.
Jumla ya miili 224 imeopolewa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa uchukuzi mhandisi Isack Kamwelwe.
Maafisa wote wanaohusika na uendeshaji wa kivuko wamekamatwa na wanahojiwa kwa uchunguzi.
Ad
Mazishi yataendelea kufanyika pale miili ikipatikana na Waziri mkuu ataendelea kubaki kisiwani Ukara, hasa katika kushiriki mazishi ya wale ambao hawatatambuliwa na ndugu zao.
Kwataarifa zaidi Bofya HAPA
Ad