TANZANIA KUWA NA SHERIA YA MIKOPO MIDOGO MIDOGO

  • Itahusu mikopo midogo midogo kama VIKOBA na ile ya mtu binafsi kukukopesha kwa siku/wiki/ mwezi au miezi miwili, mitatu kwa riba kubwa.
  • Ili kulinda haki na wajibu ya mkopaji na mkopeshaji.
  • Ni kauli ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Alisema, “Nchi yetu kwa muda mrefu.. tumekuwa tukienda bila kwa na sheria au sera inayoongoza taasisi ndogo ndogo za fedha.. SACOS, UPATU, Sjui vyama gani.. vyama vyetu vidogo vidogo huko. Lakini hata wale wakopeshaji mmoja mmoja; Kuna watu anakuwa na kibunda chake cha pesa ili kizalishe, ngoja nikopeshe.Lakini kopesha yake, utakoma! Mimi nimeshaingia huko.. unakwenda unapigwa na sida unasema pesa ya chapchap nitaipata pale.. unakwenda kwanza anataka umuwekee ..dhamana.. awake dhamana; Lakini malipo yeke ni mwezi huu.. mmoja! Na riba yake anaijua Mungu. Kwahiyo hayo yote yamekuwa yakienda bila ya kuwa na sheria. Lakini sasa serikali tumeliona hilo. Serikali zote mbili tumeona hilo. na nadhani kwa upende wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sio Bunge linalokuja.. linalofuata; Sheriff ya Taasisi ndogo za Fedha, itatungwa.’

Tazama video ya Makamu wa Rais

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAKAZI WA PEMBEZONI MWA BAHARI WAELIMISHWA ATHARI ZA MAGENDO

Wakazi na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi katika kata za Somangila, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *